Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 17 December 2014

SERENGETI BREWERIES YAZINDUA CHUPA MPYA “TUSKER 330 ML” SOKONI

Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakisikiliza jambo wakati wa uzinduzi wa Chupa mpya ya Tusker yenye mililita 330, katika halfa iliyofanyika jana katika ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi Masoko wa kampuni ya bia Serengeti, Bw. Ephraim Mafuru, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chupa mpya ya bia ya Tusker yenye ujazo wa milimita 330, hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.

Wahudumu wa kampuni ya bia ya Serengeti wakionyesha mwonekano wa chupa mpya ya bia ya Tusker yenye ujazo wa ml 330 . 

Kikundi cha sanaa cha Dar es Salaam Dance International (DDI) kikifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa chupa mpya ya bia ya Tusker. 

Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti wakiwaonyesha waaandishi wa habari (hawapo pichani), mwonekano mpya ya Bia ya Tusker yenye ujazo wa mlimita 330.

Meneja masoko-Familia ya bia ya Tusker na Pilsner kampuni ya bia ya Serengeti, Anitha Msangi akiongea na waandishi wa habari , mara baada ya uzinduzi wa chupa mpya ya Tusker yenye ujazo wa mililita 330.

Meneja masoko-Familia ya bia ya Tusker na Pilsner kampuni ya bia ya Serengeti, Anitha Msangi akiongea na waandishi wa habari , mara baada ya uzinduzi wa chupa mpya ya Tusker yenye ujazo wa mililita 330. 

Tunafurahia mwonekano mpya wa chupa ya bia ya Tusker. 

Meneja masoko wa familia ya bia ya Tusker na Pilsner, Anitha Msangi (kushoto) na Mkurugenzi wa masoko, Bw. Ephraim Mafuru (katikati) na Meneja ubunifu wa bidhaa zote za kampuni ya bia ya Serengeti Ms. Attu Mynah (kulia) wakionyesha chupa mpya ya bia ya Tusker kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).

Wateja wa bia ya Tusker Lager kwa mara nyingine wamepewa heshima baada ya kampuni ya Serengeti Breweries kuingiza sokoni chupa ya bia mpya inayojulikana kama “Tusker ml330”

Chupa hii mpya imezinduliwa jana -Golden Jubilee Tower iliyoko jijini Dar Es Salaam mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Masoko wa SBL Bwana Ephraim Mafuru pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Bw. Ephraim Mafuru alisema “Mazingira ya kibiashara ya sasa yanatulazimu kufikiria zaidi ili kuhakikisha kwamba tunaambatana na uhalisi katika soko huku tukihakikisha kwamba tunamridhisha mteja wetu katika Nyanja zote”.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa familia ya Tusker na Pilsner Serengeti Breweries Ms. Anitha Msangi alisema… “Ninaamini kwamba ubunifu unainua nia na uhitaji kwa wateja. Hivyo basi matarajio yangu makubwa ni kwa wateja wetu kuipokea na kuinunua chupa hii mpya kwa wingi.” Anitha aliongeza kwamba chupa hii ya bia itapatikana na kuuzwa nchi nzima na tutahakikisha kwamba wateja wote wanaipata bila usumbufu.

Bidhaa hii mpya ina ujazo wa ml 330 na itauzwa kwa bei ya Shilingi 2,300/= kwa bei ya rejareja. Uzinduzi wa chupa hii mpya upo katika mtazamo wa kampuni wenye lengo la kwenda sambamba na hali ya soko.

Tusker ml330 imeongezeka katika idadi ya vinywaji vilivyozinduliwa na kampuni ya SBL msimu huu ikilenga kutimiza adhima ya kuingiza bidhaa mpya katika soko la Tanzania. Bidhaa hizo ni pamoja na:-Serengeti Platinum, Jebel Coconut and Serengeti Platinum ml330

Uzinduzi wa Tusker ml 330 umekuja katika msimu wa kampeni ya Tusker FanyaKweli ambayo ina lengo la kuwahamasisha watanzania kutengeneza maisha ya baadae ambayo wote tutajivunia kwa vitendo wakati huohuo wakijifunza kupitia watu waliopata mafanikio kupitia yale waliyokuwa wakiyafanya.

KUHUSU SERENGETI BREWERIES LIMITED

Serengeti Breweries Limited inajihusisha na utengenezaji, uandaaji, uuzaji na usambazaji wa vinywaj ivya kimea na shayiri n auwele hapa Tanzania.

Premium Lager, Serengeti Platinum, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Uhuru Peak Lager, Pilsner Lager, Senator, The Kick na Guinness®..

No comments:

Post a Comment