Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 4 August 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MTUKUFU AGA KHAN IKULU DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mwanzilishi na Mwenyekiti  wa Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan Duniani, His Higness Prince Karim Aga Khan, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Agosti 3, 2014 kwa mazungumzo. Mtukufu Aga Khan yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku nne, ambapo pia atatumia fursa hiyo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Aga Khan ‘New Compass of Aga Khan University’ kinachojengwa jijini Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwanzilishi na Mwenyekiti  wa Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan Duniani, His Higness Prince Karim Aga Khan, wakati alipowasili Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam jana Agosti 3, 2014 kwa mazungumzo. Kulia ni Mbunge Tabora Kaskazini, Shafin Sumari. Mtukufu Aga Khan yupo nchini kwa ziara binafsi ya siku nne, ambapo pia atatumia fursa hiyo kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo ya Taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kukagua mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Aga Khan ‘New Compass of Aga Khan University’ kinachojengwa jijini Arusha.

Source: Michuzi Blog

No comments:

Post a Comment