Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 4 August 2014

BENKI YA NBC YATOA MKOPO WA SHS BILIONI 100 KWA MOHAMMED ENTERPRISES

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto) akisaini hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100 na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohamed Enterprises Ltd (METL), Mohamed Dewji kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni baadhi ya watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji wakionyesha mikataba muda mfupi baada ya kusaini  hati za makubaliano ya mkopo wa shs bilioni 100  kwa ajili ya kampuni dada ya METL ya Star Oils inayoshughulika na biashara ya uagizaji na usambazaji mafuta. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya maofisa wa benki ya NBC katika hafla hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Bi Mizinga Melu akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano ya kuipatia kampuni ya Star Oils mkopo wa takribani sh bilioni 100 ili kuongeza ufanisi katika kampuni hiyo ya uagizaji na usambazaji wa mafuta nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa nne kushoto), Ofisa Mtendaji Mkuu wa METL, Mohamed Dewji (wa nne kulia), watendaji wakuu wa NBC, METL na Star Oils wakipozi kwa picha ya kumbukumbu mara baada ya utiaji saini makubaliano hayo.

No comments:

Post a Comment