August 4, 2014, Dar es Salaam – Benki
ya Barclays Tanzania imezindua mpango wa kuboresha huduma zinazotolewa na benki
hiyo kwa kuweka dhamana katika huduma zake.
“Siku zote tunahakikisha mteja anapoingia katika benki yetu
anapata huduma bora kama anavyotegemea na kwa kupitia dhamana hii ya huduma
tunatoa ahadi kuwa huduma zetu zitakuwa bora maradufu. Kwa kuanzia, mteja
yeyote atakayeomba kadi ya ATM, atapatiwa katika muda usiozidi dakika ishirini
na vile vile kwa wanaohitaji vitabu vya hundi watapatiwa ndani ya siku tano,
viwango hivi ni vya juu sana katika soko letu. Lakini pia, pale tutakapogundua kuwa mteja hakupata huduma
kama tulivyomuahidi tutahakikisha tunamlipa fidia ndani ya masaa 24,” alielezea
Bw Kitoi.
“Nia yetu ni kuwa
benki inayotoa huduma haraka zinazostahili kwa wateja wetu na tutaendelea kuleta
mabadiliko mbalimbali yenye nia ya kuboresha huduma, ziwe za kisasa ili
kutimiza azma yetu ya kufanya huduma za benki kuwa rahisi kupatikana na kwa
haraka na hivyo kuwapa wateja wetu muda zaidi wa kushughulikia biashara
zao,” alielezea zaidi Bw Kitoi.
No comments:
Post a Comment