Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 2 May 2014

BAYPORT YAZINDUA BIMA YA ELIMU

Bayport yazindua Bima Ya Elimu, kwenye hafla ndogo kwenye ofisi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Kuanzia mkono wa kushoto katika picha ni Mhe. Sophia Simba (Waziri) akifutiwa na wawakilishi wa Bayport Financial Services Maneja Masoko Ngula Cheyo na Matthew Mbaga, Meneja wa Bima.

***********************************************************************************************************
Bayport Financial Services, ambayo ni moja kati ya wakopeshaji wakubwa kwa ajili ya wafanyakazi imezindua mpango wa bima kwa ajili ya elimu. Mfumo huo wa bima ni kwa ajili ya kuendeleza elimu kwa watoto pale ambapo wazazi wao wanafariki. Kwa kiwango cha chini cha TZS 2,500 kwa mwezi, bima hii ni nafuu kwa wafanyakazi wenye kipato cha chini na inamhakikishia mwanafunzi kupata mahitaji yake ya msingi katika elimu.

Akiongea katika ufunguzi wa huduma hii mpya jana, Meneja Masoko wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo aliwaeleza waandishi wa habari kwamba lengo la kubuni huduma hii ni kutokana na kuwepo kwa pengo kwenye soko la huduma ambayo inakidhi watu wenye kipato kidogo. ‘Kuwepo kwetu hapa Tanzania kwa muda mrefu kumetupa fursa ya kutambua kuwa huduma ya bima haiwafikii watu wengi na huduma hii ingewanufaisha watanzania wengi ambao wanajali watoto wao’, alisema Ngula.

Katika uzinduzi huo uliofanyika ofisini kwake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia na Watoto, Meshimiwa Sophia Simba, aliisifu kampuni ya Bayport Financial Services kwa kuzindua huduma hii ambayo itasaidia kupunguza mzigo kwa ndugu wa mfiwa na kuhakikisha motto anaendelea na elimu yake. ‘Elimu ni haki ya kila mtoto na huduma hii itapunguza wanafunzi ambao wanaacha shule kwa sababu ya kushindwa kulipa ada pindi wazazi au walezi wao kufariki. Elimu inasaidia watanzania wengi kujikomoa na umasikini na kusiwe na pingamizi yoyote kwa mtoto kutoipata,’ alisema Mheshimiwa Simba.


Wazazi na walezi wanauwezo wakuchagua jinsi ya kulipa na idadi ya wanafunzi wanaotaka kuwalipia bima hii. Bima hii inapatikana katika matawi yote ya Bayport ambayo yamesambaa katika mikoa yote hapa nchini. Matthew Mbaga ambaye ni Meneja wa Bima pia alieleza waandishi pia umuhimu na manufaa ya bima hii katika uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment