Blog Rebranding Teaser_030826

Blog Rebranding Teaser_030826

Absa Banner_301026_111126

Stanbic Bank Banner_201026

Saturday, 21 November 2026

VODACOM YAWAWEZESHA VIJANA WA UDSM KUTUMIA TEKNOLOJIA NA HUDUMA ZA KIFEDHA ZA KIDIJITALI

Afisa wa Huduma Mpya za Kifedha wa Vodacom M-Pesa, Sylivester Lukeka (kulia), akiwapa maelekezo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika chuoni hapo Novemba 20, 2026.

Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania iliwahamasisha wanafunzi wapya kutumia teknolojia na huduma za kidijitali kama nyenzo muhimu za kujenga ujuzi, kujiongezea kipato na kujiandaa kwa fursa za ajira na ujasiriamali.

Aidha, kampuni hiyo iliwatambulisha wanafunzi katika mpango wa TECHSTART, unaowawezesha kupata mafunzo mbalimbali ya Microsoft bila malipo kwa lengo la kuwajengea ujuzi wa kidijitali.

Sambamba na hilo, wanafunzi walielimishwa kuhusu huduma ya M-Wekeza ya Vodacom M-Pesa, inayowapa fursa ya kuanza kuwekeza na kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya Vodacom Tanzania ya kuwawezesha vijana kushiriki na kunufaika na fursa zinazotokana na ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini.
Afisa wa Huduma Mpya za Kifedha wa Vodacom M-Pesa, Sylivester Lukeka (kushoto), akisikiliza swali kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa majadiliano yaliyofanyika katika hafla ya UDSM Freshers Connect, Novemba 20, 2026.

Kupitia majadiliano hayo, wanafunzi walipata ufafanuzi kuhusu huduma ya M-Wekeza na fursa za kujenga ujuzi wa kidijitali kupitia mpango wa TECHSTART. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Vodacom Tanzania za kuwaandaa vijana kutumia fursa zinazopatikana katika sekta za ajira na ujasiriamali, pamoja na kunufaika na ukuaji wa uchumi wa kidijitali.
Mkuu wa Idara ya Bei za Bidhaa na Makundi Maalumu ya Wateja wa Vodacom Tanzania, Gemma Vedasto Kamara (kulia), pamoja na Afisa wa Huduma Mpya za Kifedha wa Vodacom M-Pesa, Sylivester Lukeka (kushoto), wakimkabidhi zawadi mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (katikati), wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika chuoni hapo Novemba 20, 2026.
Mkuu wa Idara ya Bei za Bidhaa na Makundi Maalumu ya Wateja wa Vodacom Tanzania, Gemma Vedasto Kamara, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika Novemba 20, 2026.

Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania iliwahamasisha wanafunzi wapya kutumia teknolojia na huduma za kifedha za kidijitali kama nyenzo za kujenga ujuzi, kujiongezea kipato na kujiandaa kwa fursa za kiuchumi.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwahudumia wanafunzi katika banda la kampuni hiyo wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Novemba 20, 2026.

Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania ilitoa elimu kuhusu matumizi ya huduma zake za mawasiliano na kifedha kupitia mifumo ya kidijitali, huku ikiwahamasisha vijana kutumia teknolojia kurahisisha shughuli zao za kila siku, kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi.
Mkuu wa Idara ya Bei za Bidhaa na Makundi Maalumu ya Wateja wa Vodacom Tanzania, Gemma Vedasto Kamara (wa tano kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliokamilisha mafunzo ya muda mfupi kupitia mpango wa TECHSTART, wakati wa hafla ya UDSM Freshers Connect iliyofanyika chuoni hapo Novemba 20, 2026.

Wanafunzi hao walionesha vyeti vyao kupitia simu zao za mkononi kama ishara ya mafanikio baada ya kukamilisha mafunzo hayo, yaliyolenga kuwajengea ujuzi wa kidijitali kupitia kozi fupi za Microsoft.

Kupitia hafla hiyo, Vodacom Tanzania iliendelea kuonesha dhamira yake ya kuwawezesha vijana kwa kuwapatia fursa za kujifunza na kujiendeleza, huku pia ikiwahamasisha kutumia huduma ya M-Wekeza kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

No comments:

Post a Comment