![]() |
| Mtoa huduma wa Vodacom Tanzania akiwaeleza wateja kuhusu huduma ya Router katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nyamhongolo, mkoani Mwanza. |
MWANZA, Tanzania; Agosti 4, 2026 – Vodacom Tanzania inaendelea kuonesha dhamira yake ya kuimarisha ujumuishaji wa kifedha na matumizi ya teknolojia ya kidijitali kwa wananchi kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Nyamhongolo, mkoani Mwanza.
Katika maonesho hayo, wataalamu wa Vodacom wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za kidijitali pamoja na kusajili wateja wapya kwenye huduma za kampuni hiyo, ikiwemo huduma ya Lipa, inayorahisisha malipo kwa njia salama, ya haraka na yenye ufanisi.
Moja ya huduma zinazovutia wakulima wengi ni M-Kulima, suluhisho la kidijitali lililobuniwa kuwawezesha wakulima kupokea malipo ya mazao yao kwa urahisi na usalama. Kupitia huduma hiyo, wakulima wanaweza kupunguza matumizi ya fedha taslimu, kuongeza uwazi katika miamala yao na kupata huduma za kifedha zinazochangia kukuza shughuli zao za uzalishaji.
Huduma ya M-Kulima inaendana na jitihada za Vodacom Tanzania za kutumia teknolojia kuboresha maisha ya wananchi na kuunga mkono maendeleo ya sekta ya kilimo, ambayo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania.
Mbali na kutoa elimu kuhusu huduma za kifedha, Vodacom pia inaendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kidijitali ili kuongeza ufanisi wa biashara na kuwezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali.
Kupitia ushiriki wake katika Maonesho ya Nanenane, Vodacom Tanzania inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama mshirika muhimu katika safari ya kuwawezesha wakulima na jamii kwa ujumla kupitia huduma bunifu zinazorahisisha maisha na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Endelea kufuatilia Kitomari Banking & Finance Blog kwa habari za biashara, benki, teknolojia, kilimo na uchumi nchini Tanzania na duniani.



No comments:
Post a Comment