Foreign Exchange Rates

Absa Loan Campaign_160426

Absa Loan Campaign_160426

CRDB Bank Advert_070325

Thursday, 21 May 2026

KAMPENI YA “WEKEZA NBC SHAMBANI USHINDE” YAZINDULIWA RUNGWE NA KYELA MKOANI MBEYA

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bw Jaffar Haniu (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” inayoratibiwa na Benki ya NBC, ikilenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kimkakati ikiwemo ufuta, kokoa na kahawa wilayani humo. Wengine pichani ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Binafsi na Biashara Ndogo wa benki hiyo, Bw. Elibariki Masuke wa (wa tatu kulia), Mkuu wa Kanda ya Kusini wa NBC, Bi. Zubeider Haroun (wa pili kulia) pamoja na maofisa wengine waandamizi wa wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Bi. Josephine Manase (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” inayoratibiwa na Benki ya NBC, ikilenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kimkakati ikiwemo ufuta, kokoa na kahawa wilayani humo. Wengine pichani ni pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Binafsi na Biashara Ndogo wa benki hiyo, Bw. Elibariki Masuke (wa tatu kulia), Mkuu wa Kanda ya Kusini wa NBC, Bi. Zubeider Haroun (kulia) pamoja na maofisa wengine waandamizi wa wilaya hiyo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kyela, Wakili Florah Luhala akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.

Rungwe/Kyela, Mbeya — Mei 20, 2026 — Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi kampeni yake ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” katika wilaya za Rungwe na Kyela mkoani Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo wa kuimarisha ujumuishaji wa huduma za kifedha kwa wakulima na kuchochea maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.

Uzinduzi huo umepokelewa kwa pongezi kutoka kwa viongozi wa Serikali katika wilaya hizo, huku Wakuu wa Wilaya ya Rungwe na Kyela, Bw. Jaffar Haniu na Bi. Josephine Manase, wakieleza kuvutiwa na namna kampeni hiyo ilivyolenga kuwainua wakulima kupitia huduma za bima, elimu ya fedha pamoja na suluhisho mbalimbali za kifedha zinazokidhi mahitaji ya sekta ya kilimo.

Kupitia kampeni hiyo, NBC inalenga kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kimkakati yakiwemo kahawa, kakao na ufuta kwa kuwafikia wakulima mmoja mmoja, AMCOS pamoja na vyama vikuu vya ushirika kupitia huduma maalum za kibenki, elimu ya kifedha na bidhaa bunifu zinazosaidia kukuza kilimo-biashara.

Serikali Yapokea Kwa Pongezi Kampeni ya NBC Shambani

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika hivi karibuni ambapo wilayani Rungwe hafla hiyo iliongozwa na Mkuu wa Wilaya, Bw. Jaffar Haniu, huku uzinduzi wa Kyela ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Bi. Josephine Manase. Hafla hizo zilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya ushirika, wakulima, wadau wa sekta ya kilimo pamoja na viongozi waandamizi wa NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Wateja Binafsi na Biashara Ndogo wa benki hiyo, Bw. Elibariki Masuke.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo wilayani Rungwe, Bw. Haniu aliipongeza NBC kwa kuendelea kubuni huduma za kifedha zinazowalenga moja kwa moja wakulima na kusaidia kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo ya vijijini.

Alisema huduma za bima zinazotolewa kupitia kampeni hiyo, ikiwemo bima ya mazao, mifugo, misitu na afya, zina mchango mkubwa katika kupunguza athari za kiuchumi zinazotokana na majanga mbalimbali pamoja na kuwahakikishia wakulima usalama wa shughuli zao za uzalishaji.

Mbali na motisha ya zawadi mbalimbali zinazotolewa kupitia kampeni hii, jambo kubwa zaidi ni namna NBC ilivyogusa mahitaji halisi ya wakulima kupitia elimu ya fedha, mikopo ya kilimo na huduma za bima ambazo zitawawezesha wakulima kuongeza tija na kupanga vizuri matumizi ya mapato yao,” alisema Bw. Haniu.

Aidha, aliwahimiza wakulima kutumia fursa hiyo kwa kufungua akaunti za NBC Shambani na kujiunga na mifumo rasmi ya kifedha itakayowawezesha kupata huduma mbalimbali za maendeleo kwa urahisi zaidi.

Elimu ya Fedha na Bima Kutajirisha Sekta ya Kilimo

Kwa upande wake, Bi. Josephine Manase alisema kampeni hiyo imekuja katika wakati muafaka ambapo Serikali inaendelea kuhimiza matumizi ya teknolojia, huduma za kifedha na uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na kuinua maisha ya wakulima.

Alieleza kuwa elimu ya fedha inayotolewa kupitia kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa wakulima kuhusu umuhimu wa kuweka akiba, kutumia bima za kilimo na afya pamoja na kuwekeza katika mbinu bora za uzalishaji.

Serikali imeendelea kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha wakulima wanakuwa na uwezo wa kuzalisha kwa tija zaidi. NBC kupitia kampeni hii imeonesha dhamira ya kweli ya kuunga mkono jitihada hizo kwa kuwapatia wakulima huduma zinazowasaidia kupunguza hatari na kuongeza usalama wa kipato chao,” alisema Bi. Manase.

NBC Yaeleza Dhamira ya Kukuza Kilimo-Biashara

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika hafla hizo, Bw. Elibariki Masuke alisema NBC inaendelea kuwekeza katika suluhisho za kifedha zinazolenga kuiwezesha sekta ya kilimo kukua sambamba na dira ya Serikali ya kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa taifa.

Alisema benki hiyo imeendelea kuimarisha huduma zake kupitia mifumo ya kidijitali, elimu ya fedha, huduma za bima pamoja na mikopo maalum kwa wakulima ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uzalishaji.

Kwa upande wake, Bw. Urassa alisema kampeni hiyo itatekelezwa kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Juni hadi Septemba mwaka huu, huku ikihusisha utoaji wa mafunzo ya kifedha, huduma za uwakala wa benki, bima ya mazao na afya pamoja na mikopo ya pembejeo na zana za kisasa za kilimo.

Aliongeza kuwa kampeni hiyo pia itatoa motisha mbalimbali kwa washiriki watakaofanya vizuri, ikiwemo zawadi za simu janja, pikipiki na kompyuta mpakato kwa wakulima binafsi, AMCOS na vyama vikuu vya ushirika.

Ili kushiriki kikamilifu katika kampeni hii, wakulima wanatakiwa kufungua akaunti ya NBC Shambani na kuitumia katika miamala yao ya kila siku. Lengo letu ni kuwahamasisha kutumia huduma rasmi za kifedha ambazo zitawasaidia kuhifadhi fedha zao kwa usalama na kupata huduma bora zaidi za maendeleo,” alisema Bw. Urassa.

Wakulima Waipokea Kampeni kwa Matumaini Makubwa

Kwa upande wao, baadhi ya wakulima walioshiriki uzinduzi huo walieleza kuridhishwa na huduma zinazotolewa kupitia kampeni hiyo, wakisema kuwa akaunti ya NBC Shambani pamoja na huduma za bima na elimu ya fedha zitasaidia kuongeza ufanisi wa shughuli zao za kilimo.

Mmoja wa wakulima hao, Bi. Nuru Mwakatobe, alisema huduma hizo zimeleta matumaini mapya kwa wakulima hususan katika eneo la usalama wa fedha na kinga dhidi ya hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na majanga ya asili au changamoto za kiafya.

Akaunti ya NBC Shambani imetengenezwa kwa kuzingatia mahitaji ya mkulima. Kupitia huduma hizi tunapata urahisi wa kufanya miamala huku tukifurahia gawio kila mwisho wa mwezi, kupata taarifa za akaunti bila gharama na zaidi kunufaika na huduma za bima zinazotupa uhakika wa kuendelea na shughuli za kilimo hata tunapokumbwa na changamoto mbalimbali,” alisema Bi. Nuru.

Kwa upande wake, Bw. Urassa alisema kampeni hiyo itatekelezwa kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Juni hadi Septemba mwaka huu, huku ikihusisha utoaji wa mafunzo ya kifedha, huduma za uwakala wa benki, bima ya mazao na afya pamoja na mikopo ya pembejeo na zana za kisasa za kilimo.



 

No comments:

Post a Comment