Tanga – Benki ya Stanbic imetoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 27.2 kwa Hospitali ya Rufaa Bombo ya Mkoa wa Tanga, hatua inayolenga kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na infant radiant warmer moja, oxygen concentrator nne, mifuko ya biohazard mitatu na mashuka 200, vyote vinavyotarajiwa kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ndani ya hospitali hiyo.
Akikabidhi vifaa hivi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, aliwashauri watumishi wa sekta ya afya kutumia vifaa vizuri na kuimarisha huduma kwa wagonjwa kwa kutumia lugha nzuri. Pia aliishukuru Benki ya Stanbic kwa mchango wake katika kuboresha sekta ya afya.
Kwa upande wake, Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Tanga, Francis Fundikira, alisema:
“Mpango huu ni sehemu endelevu ya uwajibikaji wa kijamii wa Benki ya Stanbic unaolenga kurudisha fadhila kwa jamii, sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya benki hiyo ikitoa huduma nchini Tanzania.”
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dkt. Frank Shega, aliishukuru Benki ya Stanbic kwa mchango huo na kuhimiza mashirika binafsi kuendelea kusaidia sekta ya afya nchini.


.jpeg)

No comments:
Post a Comment