Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert_070325

Selcom Pesa Advert_110225

Selcom Pesa Advert_110225

Standard Chartered Advert_300125

Standard Chartered Advert_300125

Monday, 22 September 2025

NBC YAZINDUA MSIMU WA NNE WA KAMPENI YA “NBC SHAMBANI” KWA WAKULIMA WA KOROSHO MTWARA

Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, Bw. Francis Mkuti (aliyeketi), akijaribu ubora wa trekta lililotolewa na Benki ya NBC kama zawadi kuu kwa mshindi wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’. Kampeni hiyo inaratibiwa na benki hiyo mahsusi kwa wakulima wa zao la korosho katika wilaya za Tandahimba na Newala, mkoani Mtwara, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika wilayani Tandahimba. Wanaoshuhudia tukio hilo ni pamoja na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw. Rayson Foya (aliyepanda trekta upande wa kushoto), Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Robert Msunza (aliyepanda trekta upande wa kulia), Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wilaya za Tandahimba na Newala (TANECU), Bw. Karimu Chipola (aliyebaki standing katikati), pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo na wakulima.

Tandahimba, Mtwara – Septemba 19, 2025:
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua rasmi msimu wa nne wa kampeni yake ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde” kwa wakulima wa zao la korosho katika mkoa wa Mtwara, hususan wilaya za Tandahimba na Newala. Kampeni hii ni mwendelezo wa jitihada za benki hiyo katika kuchochea uzalishaji wa zao la korosho kupitia huduma bunifu na zenye manufaa kwa wakulima.

Hafla ya uzinduzi imefanyika wilayani Tandahimba ikiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya, Bw. Francis Mkuti, aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Michael Mntenjele. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya korosho, wakiwemo wakulima na viongozi waandamizi wa NBC wakiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha, Bw. Rayson Foya.

Kauli za viongozi

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Bw. Mkuti aliipongeza NBC kwa ubunifu na kujali maslahi ya wakulima nchini kupitia huduma zake za kifedha.
Zaidi nimefurahi kusikia kupitia kampeni hii wakulima wanaweza kupata mikopo ya vitendea kazi muhimu kama matrekta, pembejeo, na mikopo ya malipo ya awali. Zawadi hizi ni zana za kilimo zinazochochea uzalishaji,” alisema.

Aidha, Bw. Mkuti alisisitiza umuhimu wa huduma za bima za afya na bima za kilimo zinazojumuishwa katika kampeni hiyo, akibainisha kuwa zina mchango mkubwa katika kusaidia wakulima kukabiliana na changamoto za kiafya na hasara zitokanazo na majanga ya asili.

Kwa upande wake, Bw. Foya alisema kampeni hiyo ni sehemu ya mchango wa NBC katika kufanikisha mkakati wa serikali kupitia Ajenda ya 2010/2030, inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi 10 ifikapo mwaka 2030.
Sambamba na uzinduzi huu, tunatoa huduma mbalimbali ikiwemo ufunguaji wa akaunti zisizo na makato ya mwezi, mikopo ya zana za kilimo kwa wakulima mmoja mmoja, pamoja na mikopo kwa vyama vya ushirika (AMCOS/Union) kwa ajili ya pembejeo,” alieleza.

Manufaa ya kampeni

Akitoa ufafanuzi zaidi, Bw. Raymond Urassa (Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Wakulima) na Bw. David Raymond (Mkuu wa Masoko wa NBC) walisema kampeni hiyo inawalenga wakulima mmoja mmoja, vyama vya msingi (AMCOS), na vyama vikuu vya ushirika vinavyopitisha fedha za mauzo kupitia akaunti za NBC Shambani.

Kupitia kampeni hii, wakulima wa korosho katika Tandahimba na Newala watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo pampu za kupulizia dawa, baiskeli, pikipiki, na maguta (pikipiki za miguu mitatu). Zawadi kuu ya kampeni kwa vyama vikuu vya ushirika ni trekta jipya.

Shukrani za wakulima

Kwa niaba ya wakulima, Bw. Karimu Haji Swalehe na Bi. Sharifa Mohammed Nahunda waliishukuru NBC kwa kuandaa kampeni hiyo, wakisema imewasaidia kuongeza uelewa wa masuala ya kifedha na kuimarisha utamaduni wa kuweka akiba. Pia walieleza kuvutiwa na huduma za bima za afya na kilimo zinazojibu mahitaji muhimu ya wakulima na familia zao.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, Bw. Francis Mkuti (aliyeshika mkasi), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa msimu wa nne wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’ inayoratibiwa na Benki ya NBC mahsusi kwa wakulima wa zao la korosho mkoani Mtwara, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika wilayani Tandahimba. Wanaoshuhudia tukio hilo ni pamoja na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw. Rayson Foya (wa pili kulia), Mkuu wa Kanda ya Kusini wa benki hiyo, Bi. Zubeider Haroun (kulia), Meneja Uhusiano wa Mawakala wa Benki ya NBC, Bi. Jacquiline Sindano (kushoto), Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Tandahimba, Bw. Billygraham Minja (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wilaya za Tandahimba na Newala (TANECU), Bw. Karimu Chipola (wa tatu kushoto), na Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Mtwara, Bw. Robert Msunza.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Tandahimba, mkoani Mtwara, Bw. Francis Mkuti (aliyeshika kipaza sauti), akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wakulima wa korosho waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa msimu wa nne wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’, inayoratibiwa na Benki ya NBC mahsusi kwa wakulima wa zao la korosho katika wilaya za Tandahimba na Newala, mkoani Mtwara.
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NBC, Bw. Rayson Foya, akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wakulima wa korosho waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa msimu wa nne wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’, inayoratibiwa na Benki ya NBC mahsusi kwa wakulima wa zao la korosho katika wilaya za Tandahimba na Newala, mkoani Mtwara.
Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Wilaya za Tandahimba na Newala (TANECU), Bw. Karimu Chipola (aliyeshika kipaza sauti), akizungumza na wageni waalikwa wakiwemo wakulima wa korosho waliohudhuria hafla fupi ya uzinduzi wa msimu wa nne wa kampeni ya ‘Wekeza NBC Shambani Ushinde’, inayoratibiwa na Benki ya NBC mahsusi kwa wakulima wa zao la korosho katika wilaya za Tandahimba na Newala, mkoani Mtwara.
Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki ya NBC, Bw. David Raymond (aliyevaa kofia), pamoja na Meneja wa Benki hiyo Tawi la Lindi, Bw. Iovin Mapunda (kushoto kwake), wakifuatilia uzinduzi huo sambamba na wageni wengine waalikwa wakiwemo wakulima.
Maofisa mbalimbali wa benki ya NBC wakielezea huduma mbalimbali za benki hiyo mahususi kwa wakulima wakati wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakiwemo wakulima wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo.
Muonekano wa zawadi mbalimbali zitakazotolewa na benki ya NBC kwa washindi mbalimbali wa kampeni hiyo.
Hafla ya utambulisho wa kampeni hiyo ilifanyika wilayani Tandahimba ikiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw Francis Mkuti aliemuwakilisha Mkuu wa Wilaya Kanali Michael Mntenjele, huku ikihudhuriwa na wadau mbalimbali zao hilo mkoani Mtwara wakiwemo wakulima pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NBC Bw Rayson Foya.

No comments:

Post a Comment