- Mkuu wa Wilaya ashiriki uzinduzi wa kituo kipya cha mafuta pamoja na huduma za ziada kama vile duka la manunuzi ya mahitaji ya nyumbani, huduma za kuosha na matengenezo ya magari.
- Pia, apokea msaada wa mitungi ya gesi safi ya kupikia ya Puma Gas inayosambazwa na kampuni hiyo ili kuwanufaisha akina mama wanaojishughulisha na biashara ndogondogo za uuzaji wa chakula.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania, Bi. Fatma Abdallah ameelezea kuwa uzinduzi wa kituo hiki sehemu ya mkakati wa kampuni kuendelea kuiwezesha jamii ya Watanzania na kuwahudumia wateja wake kwa ubunifu na weledi wa hali ya juu katika maeneo mbalimbali nchini.
“Dhamira yetu kuu ni kuendelea kuiwezesha jamii ya Watanzania pamoja na kuwahakikishia wateja wanapata huduma na bidhaa bora za nishati kwa gharama nafuu na kwa viwango vya hali ya juu. Hivyo, kama sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Huduma kwa wateja sisi tumeona ni vema kufanya kwa vitendo kwa kuwasogezea huduma karibu zaidi. Uzinduzi wa kituo hiki kipya cha mafuta hautakuwa unatoa huduma za ujazaji wa mafuta pekee bali kutakuwa na huduma za ziada kama vile uoshaji wa magari, ufundi, mitungi ya gesi safi ya kupikia, vilainishi, pamoja na duka lenye mahitaji mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani,” alifafanua Bi. Abdallah.
Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania alimalizia kwa kuwasihi wakazi wa Dege Mtaa kukitumia vema kituo hiko kipya ili kurahisisha shughuli za maisha yao ya kila siku, “nawasihi wananchi wa Kigamboni kutumia fursa zitokanazo na uwepo wa kituo hiki kipya karibu na makazi yenu. Tunaishukuru serikali kwa ushirikiano endelevu na kututengenezea mazingira mazuri ya biashara ambayo yanatuwezesha kuendelea kusambaza na kuboresha huduma zetu. Kituo hiki kitakuwa kinatoa huduma masaa 24 kila siku kwa siku zote za wiki ili kuhakikisha watu hawakwami katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi.”
Mbali na kuzindua kituo kipya cha mafuta na huduma za ziada, Puma Energy Tanzania ilikabidhi msaada wa mitungi 200 ya Puma Gas. Msaada huo uliokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya unalenga kuwanufaisha wanawake wanaojihusisha na biashara ndogondogo za uuzaji wa chakula ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni kuiwezesha jamii ya Watanzania nchini kote.
About Puma Energy
Puma Energy is a leading global downstream energy business, safely providing energy in more than 35 countries. Our downstream business segments include fuels, aviation, lubricants, and bitumen. Our purpose is to energize communities and help drive growth and prosperity by sustainably serving our customers’ needs in high-potential countries around the world.
For further information visit: www.pumaenergy.com.
No comments:
Post a Comment