Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Stanbic Tanzania, Manzi Rwegasira, akizungumza wakati wa uzinduzi wa ziara ya waendesha baiskeli kuelekea Butiama 2024, ambayo inadhaminiwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na Benki ya Stanbic. Uzinduzi huu ulifanyika kama maendesho ya baiskeli ya kijamii "Pedal for Purpose," ambayo ni mwanzo wa ziara hii kuelekea Butiama. Benki ya Stanbic imechangia kiasi cha shilingi milioni 70, ambazo zitatumika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa madawati 1,500; sekta ya afya kwa kuanzisha kliniki zinazozunguka kuhudumia mikoa mbalimbali, na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti 50,000. Kiujumla ziara hii inategemea kuboresha maisha ya watanzania 100,000. Kilele cha ziara hiyo kitafanyika Butiama, Mkoani Mara, tarehe 14 Oktoba. |
No comments:
Post a Comment