Hayo yamebainishwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo wakati akifungua Kongamano kubwa la wafanyabiashara Afrika Mashariki "East Africa Investment Forum" lenye lengo la kuunganisha wafanyabiashara hususani watoa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati, Kongamano lililoandaliwa kwa ushirikiano na vyama vikuu vya FINTECH kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Tanzania, linalofanyika kwa Siku 2 (Septemba 12-13).
Akizungumza baada ya Ufunguzi wa Kongamano hilo, Katibu Mkuu Mtendaji wa Umoja wa Makampuni yanayotoa Huduma za Kifedha kupitia Teknolojia Tanzania (TAFINA), Bw. Shedrack Kamenya amesema zaidi ya Wawekezaji 10 wameshiriki Kongamano hilo, na lengo kubwa la kuwaleta pamoja watoa Huduma za Kifedha, Watunga Sera, Wawekezaji na wadau wa SEKTA ya Huduma za Kifedha barani Afrika limetimia.
Kauli mbiu yetu ni "Wekeza na Ingia Ubia", "Invest and Partner" katika utoaji wa Huduma za Kifedha, jukwaa hili limekusudia kupambanua mada mbalimbali katika eneo wa uwekezaji katika Huduma za Kifedha lakini pia tutaangazia mazingira ya kisera ambayo yatarahisisha upatikanaji wa Mitaji kwa watoa Huduma pamoja na upotevu wa fedha unaotokana na Uhalifu wa Kimtandao (Cyber Security) na maeneo mengine kadha wa kadha ambayo tutaangazia, amesema Bw. Kamenya.
Kongamano hili linaendelea kwa siku mbili, Septemba 12 & 13 Jijini Dar Es Salaam.
Kwa upande mwingine, mmoja wa washiriki wa Kongamano hili la Kihistoria, Bw. Alfred Tembo amewapongeza TAFINA kwa kuwaunganisha pamoja katika Kongamano hilo.
Kwa upande mwingine, mmoja wa washiriki wa Kongamano hili la Kihistoria, Bw. Alfred Tembo amewapongeza TAFINA kwa kuwaunganisha pamoja katika Kongamano hilo.
No comments:
Post a Comment