Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 2 July 2024

NSSF YATOA ELIMU KWA WATUMISHI WANAOTARAJIA KUSTAAFU

Mrisho Mwisimba - Meneja NSSF Ilala.

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii NSSF umewataka watumishi wanaotarajiwa kustaafu kuanza kujiandaa ikiwa ni pamoja na kuhakiki taarifa zao za msingi sambamba na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hali itakayosaidia kupunguza changamoto za maisha pindi wanapostaafu

Rai hiyo imetolewa na meneja wa mafao wa NSSF Ilala wakati akimuwakilisha mkurugenzi wa uendeshaji NSSF Mrisho Mwisimba wakati wa warsha iliyolenga kutoa elimu kwa watumishi wanaotarajia kustaafu kutoka katika mkoa wa Temeke ambapo pia amewasisitiza kuanzisha miradi salama ya uwekezaji ili kuwa na uhakika wa kipato endelevu.

Emmanuel Nyange, Meneja Idara ya Biashara wa Benki ya Biashra ya Taifa (TCB).

Kwa upande wake Emmanuel Nyange meneja idara ya biashara wa benki ya biashra ya taifa TCB , ambao pia walihudhuria mafunzo hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha katika mafao amesema kuwa ,tcb imeamua kusimama na wastaafu kwa miaka 10 sasa ikijikita katika kutatua changamoto wanazokutana nazo wastaafu kwa kuanzisha akaunti maalumu ya Kivulini isiyo na makato yeyote wala gharama za uendeshaji,lengo likiwa ni kumnusuru mstaafu.

Nyange ameongeza kuwa Sambamba na hayo tcb imeanzisha huduma za pesheni advance inayomuwezesha mstaafu kupata fedha ya kujikimu kwa kutoa suluhu kwa tatizo analokutuna nalo,ila pia kuna huduma ya mkopo usio na masharti yeyote


Aidha kwa wastaafu watarajiwa tcb wanatoa huduma za fixed akaunti huku asilimia yake ikiwa ni mpaka asilimia 11 kwa mwaka, kupitia akaunti ya kivulini bado wastaafu wakipata majanga au ulemavu wa kudumu wanapewa fidia,na sababu kuu ni adhimio la serikali kuweza kufikia makundi yote katika huduma za ujumuishaji wa kifedha,

Huduma hizo zote zinatolewa katika mkitadha wa kutatua changamoto wanazopitia wastaafu hivyo kuwasihi wastaafu watarajiwa kuhakikisha wanasamehe na kuachana na yaliyopita na zaidi wafungue akaunti na tcb ili waweze kupata huduma zote hizo


Kwa upande wake Afisa Mafao mkuu wa NSSF Shakira Masoli amewasisitiza watumishi kujiandaa kustaafu kwa kuhakikisha wanapeleka na wanahakiki taarifa zote za msingi ili kuepusha usumbufu pindi wanapostaafu

Naye mmoja wa wanufaika wa NSSF Damas Nungu ameutaka mfuko huo kupunguza kikokotoo cha awali anachopewa mstaafu huku akiwahimiza waajiri kupeleka michango ya watumishi wao kwa wakati

No comments:

Post a Comment