Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 13 May 2024

HATI FUNGANI YA NMB JAMII YAANZA KUUZWA SOKO LA HISA LONDON


Benki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya mitaji kimataifa kwa kuiorodhesha Hati fungani ya NMB Jamii (NMB Jamii Bond) katika Soko la Hisa la London (LSE).


Hatua hiyo inaifanya Benki ya NMB kuwa taasisi ya kwanza Tanzania kuwa na hati fungani katika soko hilo na Benki ya Kwanza Afrika Mashariki kuorodhesha Hatifungani ya Uendelevu katika Soko la Hisa la London.


Hati Fungani ya NMB Jamii inalenga kuchochea uwekezaji katika miradi yenye tija kijamii na kimazingira, na toleo la Dola za Kimarekani Milioni 73 ndio limeorodheshwa kwa wawekezaji wa Soko la Hisa la London.


Uzinduzi wa mauzo ya Hati fungani ya Jamii ulifanyika wakati wa ufunguzi wa shughuli za wiki hii za Soko la Hisa la London, na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mbelwa Kairuki; Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi. Ruth Zaipuna; Mhazini wa Benki ya NMB, Aziz Chacha; Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la London, Julia Hoggetts na viongozi wengine waandamizi kutoka Serikali ya Uingereza na taasisi mbalimbali.


“Tulianza kwa kuiorodhesha hati fungani hii katika Soko la Hisa la Dar es Salaam mwaka jana, Soko la Luxembourg mwezi uliopita, na leo tunaiorodhesha hapa Soko la Hisa la London ili kuwapa wawekezaji wanaozingatia uendelevu, fursa ya kuchangia mabadiliko huku wakipata faida nzuri ya uwekezaji wao,” Bi Zaipuna alieleza.


Bi Zaipuna alisema masoko ya kimataifa yanaiwezesha benki ya NMB kuwa na wigo mpana wa kupata fedha kwa ajili ya kufadhili miradi inayosaidia kuboresha mazingira, kubadilisha jamii na kuwa na mustakabali bora kwa watu wote.

“Mafanikio haya kipekee yanadhihirisha imani waliyonayo wawekezaji wa Kitanzania na wa Kimataifa katika uthabiti wa Benki ya NMB na dhamira yake ya uendelevu katika utendaji wake, biashara, jamii na masuala ya mazingira,” Bi Zaipuna alisema.

#NMBKaribuYako 
#NMBJamiiBond

No comments:

Post a Comment