Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Samalu akiwakaribisha wanawake wajasiriamali kwenye semina ya mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’ . |
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Ecobank Tanzania, Joyce Ndyetabura akizungumza kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wanawake pamoja na wajasiriamali waliofika kwenye semina hiyo. |
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Kati (SME) wa Ecobank Tanzania, Juma Hamisi akizungumza kuhusu namna ya kufungua akaunti kwenye Benki hiyo. |
Mkufunzi ambaye ni Mkuugenzi wa Kampuni ya TAPBDS, Joseph Migunda akitoa mafunzo ya ujasiriamali na namna wanavyoweza kuimarika katika ukuzaji wa mitaji kwenye mauzo na ununuzi. |
Mpango huo ni maalum kwa Benki hiyo kuwaelimisha Wanawake hao jinsi ya kufanya biashara hizo sambamba na kuwapa mikopo kwa bei nafuu. Ili kuwa na vigezo ni lazima Wanawake hao Wajasiriamali wawe na Leseni za Biashara na kufungua Akaunti katika Benki hiyo.
Akizungumza wakati wa kufungua Semina hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Charles Asiedu amesema mpango huo ni maalum ambao utawafikia wanawake wajasiriamali wengi na kuongeza mtaji wao, kupata faida na kujinua kiuchumi.
Pia amesema Ecobank imeanzisha mfumo maalum wa kuwaunganisha wafanyabiashara mabalimbali barani Afrika ujulikanao kama "Trade hub" wanatumia Benki hiyoikiwa na lengo la kupanua wigo wa biashara zao ili kuweza kutanuka kimasoko kimataifa na kuwakutanisha wafanyabiashara mabalimbali ili kuweza kuuza na kununua bidhaa mbalimbali kupitia huo mfumo.
Amesema kutokana na Takwimu za Benki hiyo zaidi ya asilimia 95 ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa hapa Tanzania ni asilimia 54 zinayomilikuwa na wanawake hivyo mpango huo utaweza kuwainua wanawake wengi ili kuweza kujitegemea kwenye mitani ikiwemo na kukua kiuchumi
"Tangu kuzinduliwa kwa mpango maalum ujulikanao kama ‘Ellevate by Ecobank’, Ecobank Tanzania imewafikia wanawake zaidi ya 200 ambapo mpaka mwishoni mwa mwaka huu wanatarajia kuwafikia wanawake wafanyabiashara 500" alisema Asiedu
Ellevate by Ecobank inalenga Biashara zinazomilikiwa na wanawake, Biashara zinazoendeshwa na wanawake, Kampuni zenye asilimia kubwa ya wanawake kwenye ngazi za maamuzi kwenye kampuni hizo, Kampuni zinazozalisha bidhaa za wanawake kama vile urembo, mavazi nk.

No comments:
Post a Comment