Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 22 March 2024

BENKI YA DCB YAANDAA FUTARI KWA MADIWANI WA JIJI LA DAR ES SALAAM


Benki ya Biashara DCB ilipata fursa ya kipekee ya kuandaa hafla fupi ya futari kwa Waheshimiwa Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, Mgeni rasmi akiwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mh. Omar Kumbilamoto.


Kikao hicho kilikuwa ni sehemu ya jitihada zetu za kuimarisha ushirikiano na Halmashauri zetu, huku tukijadiliana kuhusu fursa za pamoja.


Mhe. Kumbilamoto aliishukuru Benki na kutoa pongezi kwa kikao hicho kwani kimewakutanisha pamoja Madiwani wote na Uongozi wa Benki katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa ramadhan.


Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshingi aliwashukuru Waheshimiwa Madiwani kwa kuitikia wito na kujumuika pamoja nasi kwani utamaduni huu unadumisha umoja na ushirikiano baina yetu. 


Umoja wetu ni nguvu yetu!

No comments:

Post a Comment