Kila Mtanzania sasa anaweza kumiliki simu ya kisasa yenye kasi ya 4G, iliyotengenezwa na teknolojia ya kisasa kama vile mfumo wa malipo ya "Tap pay" ambao hii simu itawezeshwa nayo, pia ikiwa na programu zote maarufu za mitandao ambazo zinaifanya TZ1 kuwa juu kulinganishwa na simu nyingine za rika lake; kuthibitisha ahadi ya Y9 Microfinance ya kutoa huduma za mikopo ya simu kwa watu wote. Zaidi ya hayo, Y9 Microfinance inaingia sokoni, kuvunja vizuizi na kuwezesha ufikiaji wa kidijitali wa 4G na huduma za kifedha kwa watu wote.
Huduma za mikopo wa Simu huwa ni nafuu kwa watu ambao huona gharama ya kununua simu janja ni kikwazo. Kwa kuongeza TZ1 ni ya kisasa na yenye kasi ya 4G, na ni bei nafuu. Y9 Microfinance pia hutoa huduma kama vile mikopo ya pesa taslimu, mikopo ya fedha za matumizi na mikopo ya mshahara kidigitali, kupitia simu janja. Y9 Microfinance, inalenga kuwezesha idadi kubwa ya watu, kutumia na kunufaika na kasi ya mtandao, huduma za kidijitali kwa ukuaji wa kibinafsi na kifedha. Huduma ya mkopo wa Simu ya Y9 Microfinance inalenga kurahisisha malengo ya kukuza matumizi ya kidijitali kote Tanzania. Taasisi inatazamia mustakabali ambapo kila mtu, bila kujali hadhi yake ya kiuchumi, aweze kuwa na zana na fursa ya kushiriki kwa maana katika uchumi wa kidijitali.
Bw. Kavinattamai alisisitiza mabadiliko haya, akiongeza, "Uzoefu wetu wa kutoa simu za mkononi zenye kasi ya 4G ulionyesha uhitaji ya teknolojia hii, tulitambua hitaji la kufikia hadhira kubwa zaidi. Huduma ya mkopo wa Simu ni jibu letu kwa hili, kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma katika mapinduzi ya kidijitali."
Y9 Inc imejitolea kupanua biashara zake za kidijitali katika nchi kadhaa za Afrika na zaidi. Na tayari wapo kwenye mazungumzo na taasisi nyingine kuboresha ushirikiano wa bidhaa za Y9 katika masoko ili kuharakisha ukuaji na kuondoa vizuizi vya kidijitali na kifedha.
Kuhusu Y9 Microfinance
Y9 Microfinance Tanzania Limited ni kampuni tanzu ya Y9 Inc USA. Y9 Microfinance, ikifanya kazi na kusimamiwa nchini Tanzania kama taasisi inayoongoza kutoa mikopo midogo, inatoa suluhisho la kifedha kwa watu binafsi, SMEs, na makampuni makubwa. Y9 Inc imejitolea kuleta athari chanya kupitia ushirikishwaji wa kidijitali na kifedha.
Mawasiliano:
Y9 Inc:
Leah Banda
Chief Impact and Brand
Leah@Y9bank.com
Y9 Microfinance Tanzania:
Sophia Mang’enya
Mkurugenzi wa Masoko
Sophia@y9bank.tz
+255767210761
Sophia Mang’enya
Mkurugenzi wa Masoko
Sophia@y9bank.tz
+255767210761
No comments:
Post a Comment