Benki ya CRDB imezindua rasmi kampeni maalum ya elimu ya bima ya vyombo vya moto iliyopewa jina la ‘Kuwa Shua’ tamasha lililofanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Akizungumza katika tamasha hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe alisema ili kuchochea ukuaji wa sekta ya bima na kuongeza ujumuishi wa sekta hii yaani “Insurance Inclusion,” Serikali kupitia Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha imekuwa ikiandaa programu mbalimbali za elimu kwa umma juu ya umuhimu wa matumizi ya bima.
"Ni imani yangu kuwa kampeni hii ya mwaka huu ya “Kuwa Shua” itawajengea uelewa wamiliki wa vyombo vya moto umuhimu wa kukata bima dhidi ya majanga yanayoweza kutokea, niipongeze Benki yetu ya CRDB kwa kutekeleza kwa vitendo agizo hili la ufikishaji wa elimu ya bima kwa wateja wenu na wananchi. Nafahamu mwaka jana mliendesha kampeni ya “Bima Unachokithamini” mkitoa elimu ya umuhimu wa bima katika nyanja mbalimbali", alisema Gondwe.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akipata maelezo kutoka kwa Maafisa wa Shirika la Bima nchini wakati alipotembea banda lao katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akifurahia jambo na Maafisa wa Shirika la Bima la Zanzibar wakati alipotembea banda lao katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akipata maelezo kutoka kwa Mdau mkuu wa ukarabari wa magari, Edwin Mactemba wakati alipotembea banda lake katika tamasha la kutoa elimu ya bima kwa vyombo vya moto lililoandaliwa na Benki ya CRDB na kufanyika kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment