- Walimu na wanafunzi watakiwa kutumia fursa za kimtandao kuendana na kasi ya kidigitali
Hayo yalibainishwa jana katika warsha maalumu iliyoandaliwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kujadili juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuboresha elimu visiwani humo na kuhudhuriwa na wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali na kufanyika katika Ukumbi wa Taasisi uliopo Vuga.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Meneja Chapa wa Zantel kwa niaba ya Mkuu wa Zantel-Zanzibar,David Maisori alisema warsha hiyo ililenga kujadili kiundani namna gani wadau wa elimu wanavyoweza kutumia intaneti kuendeleza na kuboresha utendaji kazi katika sekta hiyo.
“Kampuni yetu ya Zantel imefanya kazi kubwa sana ya kujenga miundombinu ya mtandao wenye kasi wa 4G hapa Zanzibar. Tuna minara zaidi ya 100 inayotoa huduma ya mtandao wa 4G kote Unguja na Pemba hivyo kazi ni kwenu sasa wanafunzi, walimu na wahadhili, serikali, taasisi na wadau wengine wa elimu kutumia miundombinu iliyopo ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia,” alisema.
Alisema wanafunzi wana uwanja mpana zaidi wa kuendeleza taaluma zao kwani kupitia mtandao wanaweza kufanya mambo mengi zaidi ya kuwanufaisha kielimu mbali na kutumia katika mitandao ya kijamii pekee.
“Kwa kutambua hilo, Zantel tuna simu za bei nafuu zaidi aina ya SMARTA inayouzwa kwa Sh39,999/= tu pamoja na vifurushi vya wanafunzi ili tu kuhakikisha wanafunzi wanapata intaneti ya uhakika kwaajili ya kujisomea na kupeana taaraifa mbalimbali,” alisema.
Naye, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Omari Saidi Ali alisema Serikali imefanya juhudi kubwa kuboresha miundombinu ikiwamo kujenga mkongo wa Taifa mawasiliano na minara ya mawasiliano ili kuhakikisha huduma zinakuwa za uhakika na nafuu.
“Tumefanya jitihada hizi ili nchi yetu iendane na karne ya maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na kuanzisha tume mbalimbali za usimamizi.Lakini pia tumeweka sera ikiwamo sera ya Serikali mtandao ili kuchochea matumizi ya mtandao,”
Alitolea mfano kipindi hiki ambacho dunia imekumbwa na ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo mtandao umegeuka kuwa nyenzo muhimu ya mawasiliano hasa kwa kufundishia kutokana na shule kufungwa hivyo kufanya intaneti kuwa mkombozi mkubwa katika kuendeleza elimu.
Aliipongeza Zantel kwa jitihada za kuhakikisha mtandao wa 4G unawafikia watu wengi zaidi pamoja na unafuu wa huduma zake ikiwamo kwa wanafunzi.
Kwa upande wake, Mhaddhiri wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere-Zanzibar, Dk.Venance Kalumanga alisema mbali na kujifunza, wanafunzi wanaweza kutumia mtandao kujiendeleza kibishara ili kuepukana na tatizo la ajira mara baada ya kuhitimu.
No comments:
Post a Comment