Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Monday, 2 August 2021

MAPATO YA EABL YAENDELEA KUKUA PAMOJA NA MAZINGIRA MAGUMU YA BIASHARA

Mkurugenzi Mtendaji wa EABL Group, Jane Karuku.

Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) imepata ongezeko la mapato la aslimia 15 kufikia shilingi za Kenya bilini 86.0 kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2021. Faida kabla ya kodi iliongezeka kwa aslimia 2 kufikia shilingi za Kenya 10.9 bilioni. Ukuaji wa faida usioridhisha umechangiwa na gharama za mfumuko wa bei, ubadilishaji wa fedha na gharama za kodi. 

Mafanikio haya yameweza kufikiwa wakati kukiwepo mazingira magumu ya biashara. Kampuni iliweza kufanya mabadiliko yaliyoendana na tabia zilizobadilika za wateja ikiwa ni pamoja na biashara kwa njia ya mtandao, kuwapelekea wateja bidhaa sehemu walipo na kuweka vifungashio vya kuondoka na bidhaa

Dondoo za masoko kwa mwaka huu wa fedha:
  • Kenya: Kenya Breweries Limited (KBL) imeweza kupata ukuaji wa mapato wa 10% mwaka baada ya mwaka. Mafanikio haya yametokana na kuweza kuangalia mahitaji kwa wakati husika na kutumia njia mpya kuwafikishia bidhaa wateja wakati uwekezaji ukiendelea kufanyika kwenye bidhaa za kimkakati zaidi.
  • Uganda: Uganda Breweries Limited (UBL) mapato yamekua kwa asilimia 33 mwaka baada yam waka wakati bia na pombe kali zionyesha ukuaji mzuri zaidi. Ukuaji huo ulitokaa na kuendesha biasahara kulingana na mazingira mapya ikiwa ni Pamoja na kubadilisha mbinu za kufikisha bidhaa sokoni. Uganda iliwekeza kwenye upanuzi katika uzalishaji kusaidia mauzo yanayokua ikiwa ni sehemu ya mkakati wa EABL
  • Tanzania: Serengeti Breweries Limited (SBL) mapato yake yamekua kwa asilimia 15 huku bia na pombe kali vikionyesha ukuaji mzuri wa namba mbili (double digit). Ukuwaji huo mzuri umetokana na uwekezaji kwenye bidhaa pamoja na upanuzi katika uzalishaji kwa bia pamoja na uzalishaji wa pombe kali. 
Faida ya EABL baada ya kodi katika kipindi hiki imeshuka kwa asilimia 1% kufikia shilingi za Kenya Bilioni 7 kutokana na kuathiriwa mfukumo wa bei, kodi na atahri za ubadilishaji wa fedha za kigeni. Unafuu wa kodi uliotolewa Kenya kutokana na ugonjwa wa COVID-19 uliishia Disemba 2020 na kupelekea kurudi kwa kodi iliyokuwepo kabla ya Covid-19

Katika kipindi hiki kipaumbele cha kampuni kilikuwa ni kuhakikisha afya na usalama wa watu kwa kuwapatia vifaa vilivyowawezesha kufanya kazi katika mazingira salama.

Mkurugenzi mtendaji wa EABL Group Jane Karuku, alisema: “Mwaka wa fedha 2021, umekuwa mgumu kutokana na ugonjwa wa Covid-19 kuathiri biashara katika eneo lote la Afrika Mashariki. Kenya na Uganda ziliweka hatua kali za udhibiti na watu walipunguza matumizi yasiyo ya lazima jambo ambalo lilituathiri. Tuliweza kukabliana na hali hii kwa kuwekeza kwenye bidhaa, kuongeza uzalishaji na kuendeleza jitihada za ili kupunguza matumizi na kuhakikisha tunaendelea kuwa imara,”

Akizungumzia kuhusu mipango ya mbele Jane alisema “tunafahamu kuwa athari zinazoletwa na Corona zitaendelea. Hata hivyo, tuna uhakika kuwa mkakati wetu wunafanya kazi vizuri na tutaendeleza jitihada za kuimarisha biashara,”

No comments:

Post a Comment