Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 21 December 2020

WIZARA YA MAZINGIRA YASHIRIKIANA NA VODACOM TANZANIA FOUNDATION KUZINDUA MSITU WA KUPANDWA ULIOKO MEDELI JIJINI DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu (kushoto) akifunua kitambaa kwa kushirikiana na Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua (wakwanza kulia) kuashiria uzinduzi rasmi wa bustani ya msitu wa miti ya kupandwa eneo la Medeli Jijini Dodoma hivi karibuni. Jiji hilo limetenga eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya msitu huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Ummy Mwalimu akipanda mti kwa kushirikia na Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. David Mwamfupe wakati wa kuzindua msitu wa miti ya kupandwa uliopo eneo la Medeli Jijini Dodoma hivi karibuni. Kulia anayeshuhudia ni Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua.
Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua (kushoto) akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. David Mwamfupe walipokutana kwenye uzinduzi wa msitu wa kupandwa eneo la Medeli Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais , Mazingira, Ummy Mwalimu (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua walipokutana kwenye uzinduzi wa msitu wa miti ya kupandwa eneo la Medeli Jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua (katikati) Emanuel Medukenya (kushoto) na Ibrahim Salumu (kulia) wakibeba miti kwa ajili ya kupanda eneo la Medeli Jijini Dodoma kwenye msitu wa miti ya kupandwa.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom, Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Grace Chambua (katikati) Emanuel Medukenya (kushoto) na Ibrahim Salumu (kulia) wakishirikiana kupanda miti eneo la Medeli Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa msitu huo wa miti ya kupandwa wenye ukubwa wa ekari 10.

No comments:

Post a Comment