Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 22 December 2020

BENKI YA I&M YAMALIZA MWAKA KWA STAILI YAKE, YAANZISHA HUDUMA YA RAFIKI CHATBANKING INAYOMUWEZESHA MTEJA KUPATA HUDUMA ZA KIBENKI KWA NJIA YA WHATSAPP

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Baseer Mohammed (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Wateja wa Rejareja, Lilian Mtali (wa nne kulia) pamoja na baadhi ya wateja wa Benki hiyo wakizindua huduma mpya ya Rafiki ChatBanking ambayo inawawezesha wateja kupata huduma za kibenki kwa urahisi zaidi kwa njia ya WhatsApp kwenye simu yake ya mkononi.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya I&M, Baseer Mohammed (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Rafiki ChatBanking ambayo inawawezesha wateja kupata huduma kwa urahisi zaidi kupitia WhatsApp. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja wa Rejareja Lilian Mtali, kulia ni ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa, Krishnan Ramachandran.
Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Wateja wa Rejareja wa Benki ya I&M Lilian Mtali akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Rafiki Chatbanking inayomuwezesha mtajea kupata huduma za kibenki kwa urahisi zaidi kupitia njia ya WhatsApp. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Baseer Mohammed na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa, Krishnan Ramachandran.

Dar es Salaam. Desemba 21, 2020 - Katika kuhakikisha wateja wanazifika huduma za kibenki kwa urahisi zaidi, Benki ya I&M imezindua huduma mpya ijulikanayo kama ‘Rafiki ChatBanking’ inayomuwezesha mteja kupata huduma za kibenki kwa urahisi zaidi kwa njia ya WhatsApp kwenye simu yake ya mkononi. Kupitia huduma hiyo, Benki hiyo inaendelea kudhihirisha azma yake ya kuendelea kuwa karibu zaidi na wateja kwa kubuni bidhaa na huduma bora ambazo zinampa mteja uhuru wa kifedha na kuboresha maisha.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo,Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Baseer Mohammed alisema huduma ya Rafiki ChatBanking ni ya aina yake ambayo inasogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja ili kupunguza adha ya kufuata huduma umbali mrefu kwani inampa mteja uhuru wa kufanya miamala kwa WhatsApp.

“Benki yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha inaleta huduma na bidhaa za kibunifu ambazo zinafanya maisha ya wateja wetu kuwa rahisi na bora zaidi kwa kutumia fursa mbalimbali ambazo zinaletwa na teknolojia za kidijitali,” alisema.

“Leo Tunayo furaha kuitambulisha huduma ya Rafiki Chat Banking kwa wateja wetu, huduma hii inampa mteja uhuru wa kupata huduma za kibenki mahali popote alipo kwa njia ya WhatsApp na hivyo kudhihirisha azma yetu isemayo ‘Tuko Upande Wako’, Aliongeza Bw. Baseer.

Mkuu wa Idara ya wateja wa rejareja wa benki ya I&M, Bi. Lilian Mtali alisema huduma hiyo ni salama na rahisi kutumia inayomruhusu mteja kupata huduma za kibenki zikiwamo kutuma pesa ndani na nje ya benki, kuangalia salio, kulipia bili mbalimbali pamoja huduma za kuhamisha pesa kutoka au kwenda kwenye mitandao ya simu-bank.

“Tunatambua kuwa si kila wakati wateja wanapata muda wa kutembelea benki au ATM ili kupata huduma kutokana na kuwa na majukumu na ndiyo maana tumekuja na Rafiki ChatBanking ambayo inamruhusu mteja kupata huduma zote za kibenki popote alipo huku akiendelea kufurahia kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki kwa njia ya WhatsApp,” alisema Bi. Mtali.

Ili Kujiunga na huduma ya Rafiki ChatBanking mteja anatakiwa kuhifadhi ‘save’ namba +255 755 674 696 kwenye simu janja na kisha anaweza kupata huduma yoyote ya kibenki anayohitaji kwa kutuma ujumbe mfupi kwa kuanza na neno ‘Hello’ na kisha fuata maelekezo yatakayotolewa.

No comments:

Post a Comment