Akizindua mpango huo katika hoteli ya Johari Rotana Jijini Dar es salaam hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela alisema, Mpango huo ni mahususi katika kuwawezesha wanawake wa CRDB Banki ili waweze kuwa viongozi katika nyanja mbalimbali pamoja na kuwafanya waweze kujiamini na kukamata fursa zilizopo.
Mpago huo ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani, ambapo Benki ya CRDB imeamua kuadhimisha kwa kuzindua program maalum na kuwapa semina wanawake wa Benki ya hiyo.
Aidha Nsekela alisema mpango huo utakuwa endelevu kwani Benki ya CRDB sio tu kuwa inaamini katika nafasi sawa yaani 50/50, bali imeona ni vema kuwa na mpango maalumu kwa kuwafanya wanawake wawe na wigo mpana zaidi kuweza kupambana kwa kujiamini na kushika nafasi na nyazifa mbalimbali za uongozi.
No comments:
Post a Comment