Balozi wa Finland Nchini Tanzania Riita Swan akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'My Life, My Purpose' chenye historia ya maisha binafsi ya Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa. |
Wito huo umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua kitabu cha maisha ya binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa kiitwacho 'My Life, My Purpose'.
"Napenda kutumia fursa hii, kumpongeza Rais Mstaafu, Mzee Mkapa kwa kuandika kitabu hiki na kwa mchango wake mkubwa alioutoa na anaoendelea kuutoa kwa taifa letu pia naipongeza Taasisi ya Uongozi kwa kuratibu zoezi zima la uandishi wa kitabu hiki kwa kuwa na mambo mengi mazuri" Alisema Rais Magufuli.
Mhe. Rais aliongeza kuwa kama alivyoeleza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof. Joseph Semboja kuwa jukumu la taasisi hii ni kuwaanda, kuwaimarisha na kuwaendeleza vingozi….bila shaka kuratibu na kuchapisha machapisho mbalimbali ni sehemu ya jukumu hilo hasa barani Afrika.
"Wito wangu kwenu Taasisi ya Uongozi muangalie jinsi ya kutafsiri kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili…..naomba kusisitiza viongozi wastaafu wengine waandike vitabu ili kutoa chachu kwa vijana wetu ambao watakuwa viongozi wa baadae kujifunza mambo mbalimbali, tusiishie tu kwa viongozi wastaafu katika ngazi ya Urais bali hata viongozi wengine," Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameongeza kuwa nitafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif, …….nitafurahi kusoma kitabu cha mzee Warioba…… nitafurahi kusoma kitabu cha Spika Job Ndugai kuwa nae amezaliwa kongwa.
Uzinduzi wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William Benjamin Mkapa kijulikanacho kwa jina la "My Life, My Purpose" ulihudhuriwa na Rais wa Mstaafu wa awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa na Rais wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein.
Mbali na kuzindua kitabu hicho, pia leo ilikuwa ni siku muhimu kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu, kwani leo alikuwa akisheherekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa akiwa ametimiza miaka 81 ya kuzaliwa.
Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali waliohudhuria uzinduzi wa kitabu hicho ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Balozi wa Finland Nchini Tanzania Riita Swan
Wengine ni Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu na Sayansi, Prof. Joyce Ndalichako, Mabalozi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Amon Mpanju, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, viongozi wa vyombo vya ulinzi na Usalama, wakuu wa mikoa, viongozi wa dini, wakuu wa taasisi mbalimbali na asasi za kiraia.
Awali akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuhakikisha kuwa taifa linajitegemea hasa katika maendeleo.
"Kujitegemea ni muhimu sana kama nchi, na ni muhimu kwa heshima ya taifa letu" amesema Rais Mkapa.
Foreign Affairs Blog
No comments:
Post a Comment