Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Friday 29 November 2019

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YASHAURI MFUMO WA PAMOJA WA KODI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUHARAKISHWA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Bia ya Serengeti, Mark Ocitti (wa pili kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushuru na Biashara wa Sekretariati ya EAC Kenneth Bagamuhunda akifuatiwa na Meneja wa kanda wa Coca cola na wa kwanza kulia ni David Tarimo kutoka kampuni PWC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Bia ya Serengeti, Mark Ocitti (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoa mada na wachangiaji muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Bia ya Serengeti, Mark Ocitti akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Biashara la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.
  • Asema utofauti wa kodi za ndani unasababisha kuongezeka bidhaa bandia za pombe
Arusha, Novemba 29, 2019: Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti, ameshauri kuharakishwa kwa utaratibu wa kuoanisha mfumo wa kodi kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Ocitti amesema, pamoja na kwamba hatua nzuri na kubwa imefikiwa, vikwazo vya kibiashara vilivyopo havina budi kushughulikiwa ili kuongeza kasi ya uwekezaji pamoja na kurahisisha biashara ya bidhaa na huduma miongoni mwa nchi wanachama

Akizungumza katika mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Wakuu wa Nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, Ocitti alisema tafsiri tofauti za vipengele vya kisheria kama ‘bidhaa za nje’ imesabisha kuwepo kwa kodi kubwa kwa bidhaa zinazotoka ndani ya nchi wanachama jambo ambalo limepunguza kasi ya ukuaji wa biashara.

“Utekelezaji wa kuoanisha mfumo wa kodi miongoni mwa nchi wanachama umekuwa hauendi vizuri sana kwa sababu mbali mbali ikiwamo utofauti ya kiuchumi pamoja na kufikiria suala la mapato, viwanda vya ndani, ushindani na nyinginezo,’ alisema

Akizungumzia athari zake kwenye sekta ya uzalishaji wa bia, alisema utofauti wa kodi za ndani miongoni mwa nchi wanachama, umesababisha kuongezeka kwa pombe haramu na kuongeza kuwa bado kuna changamoto katika utekelezaji wa kanuni itayoweka mfumo wa kodi unaofanana kutokana na utofauti wa maendeleo ya kiuchumi na pia hakuna msukumo wa kisheria unatoa msisitizo kwa jambo hilo.

“Kasi ndogo ya upitiaji wa Itifaki ya Ushuru wa Forodha kwa nchi wanachama wa EAC unaathiri baadhi ya shughuli pamoja na kuzifanya bajeti za nchi hizi kutegemea kwa kiasi kikubwa ushuru wa forodha. Hata hivyo, kuanzia mwaka 218 kumekuwa na mfumo mzuri kati ya nchi wanachama kwa kukuliana muundo wa 0%, 10%, 25% na 35.

Akizungumzia namna kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL) ambayo ni kampuni mama ya SBL ilivyoathirika alisema imekuwa ni bahati nzuri kuwa makampuni yaliyo chini ya EABL yamesajiliwa kama makapuni ya ndani kwa nchi wanachama na hivyo hayajaathirika sana kwa kuwa bidhaa zake zinazalishwa ndani ya nchi hizo.

“Hata hivyo, uwekaji wa viwango vya pamoja kwa bidhaa ambazo zipo tayari kwa ajili ya kutumika (RTD) imeleta shida kwa mfano kwenye biashara ya bidhaa hizo zinazotoka Kenya kuja Tanzania,” alisema

Kwa Masiliano zaidi wasiliana na;

John Wanyancha,
Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma,
Simu: 0692148857
E-mail: john.wanyancha@diageo.com

No comments:

Post a Comment