Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 31 January 2019

MKURUGENZI MKUU WA NHC ATEMBELEA ENEO JIPYA LINALOKUSUDIWA KUJENGWA MAKAZI YA WATUMISHI WAANDAMIZI NA MABALOZI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Dk Maulidi Banyani (kulia) jana alitembelea eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu. Eneo lipo karibu kabisa na ulipo mji wa Serikali kulikojengwa Wizara mbalimbali za Serikali. Pichani Afisa Miliki wa NHC Dodoma Jaffari Chege (kushoto) akimuonyesha Mkurugenzi Mkuu mfano wa michoro ya eneo hilo. 
Ukamilishaji wa ujenzi wa mji wa kiserikali ukiendelea ndani ya jengo la Wizara ya Fedha wakiwa wanafanya skimming.
Jengo la Wizara ya Fedha lilivyo sasa.

Eneo la Mtumba linalokusudiwa kuchukuliwa na NHC kwaajili ya kujenga nyumba za kuishi watumishi wa kada ya kati na juu.
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani cha Shirika la Nyumba la Taifa Abdallah Migilla (kulia) akiteta jambo na Injinia Hassan Mohammed wa Shirika la Nyumba la Taifa kwenye eneo kunakojendwa Wizara ya Viwanda na Uwekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk Maulidi Banyani (wa pili kushoto) akitembelea eneo la Wizara hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk Maulidi Banyani (kulia) akielekeza jambo. 

No comments:

Post a Comment