Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Monday 22 October 2018

WATEJA WA TIGO SASA WANAWEZA KUNUNUA MAUDHUI MTANDAONI KUPITIA TIGO PESA


Tigo Pesa na Google team waungana kuwezesha Watanzania kulipia maudhui au application yoyote inayopatikana Google Play Store
Dar es Salaam, 18 Oktoba 2018 - Je umewahi kutaka kununua muziki, cinema, apps au kusoma maudhui kwenye mtandao wa Google Play Store lakini ukashindwa kufanya hivyo kwa sababu hukuwa na kadi ya benki?

Tangu Juni ya mwaka huu, kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidigitali nchini, Tigo iliingia katika makubaliano na Google kuwapa wateja uwezo wa kulipia maudhui kutoka mtandao wa Google Play Store kwa njia ya Tigo Pesa.

Huduma hii inayowezeshwa na Bango inawawezesha wateja 7 milioni wanaotumia huduma ya kifedha ya Tigo Pesa kulipia maudhui au application yoyote inayopatikana Google Play Store kwa kutumia akaunti yao ya Tigo Pesa.

‘Wateja wa Tigo wanaotumia simu janja za Android ama tablet sasa wanaweza kufanya manunuzi ya moja kwa moja au malipo kwa njia ya kujisajili kupitia Play Store. Huduma hii inapatikana kwa njia rahisi na haraka mahali popote pale nchini kupitia Tigo Pesa. Hii inawapa wateja wetu uwezo zaidi wa kupakua na kufurahia maudhui ya kimtandao kutoka Google Play Store huku wakitumia mtandao wetu wa uhakika na wenye kasi ya juu zaidi wa 4.5G nchini,’ Mkuu wa Huduma ya Kifedha ya Mtandao wa Tigo, Hussein Sayed alisema jijini Dar es Salaam leo.

Suluhisho hili linawawezesha wateja kufurahia huduma za manunuzi ya bidhaa na huduma walizozoea kwa kuunganisha matumizi ya Google Play na Tigo Pesa. Ili kukamilisha manunuzi mteja anatakiwa kufuata hatua za kawaida za kufanya manunuzi kwenye Play Store na katika hatua ya kufanya malipo achague Tigo Pesa. Fuata hatua rahisi za kuunganisha akaunti yako ya Google na akaunti yako ya Tigo Pesa kisha unda na uingize herufi 6 za siri zitakazotumiwa kwa manunuzi yote ya Play Store.

Mahir Sahin, Mkurugenzi wa Google – Huduma za Android Barani Afrika, alisema “Tuna furaha kubwa kuungana na Tigo kuzindua ubunifu huu utakaowezesha wateja wa Tigo Pesa kufanya malipo ya moja kwa moja kwenye Googe Play Store. Hii itawezesha mamilioni ya Watanzania ambao hawana kadi za benki kufurahia huduma kamili za maudhui yanayopatikana kwenye Google Play.”

‘Tigo inaongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali na Tigo Pesa ndio kinara wa ubunifu katika utoaji wa huduma za kifedha kwa njia ya mtandao, kwa sababu ndio huduma ya kwenza kuwezesha Watanzania kununua maudhui kutoka Google Play Store. Hii inathibitisha kuwa Tigo Pesa ni huduma kamili ya kifedha inayowapa wateja huduma nyingi na bora zaidi za malipo,” Hussein aliongeza.

Idadi kubwa ya Watanzania wanapenda kutumia simu zao za mkononi kufanya manunuzi ya huduma ya bidhaa, na sasa Tigo inawawezesha kununua maudhui wanayopenda zaidi kupitia huduma inayoongoza duniani ya Tigo Pesa.

Kuhusu Tigo Tanzania
Tigo Tanzania ni kampuni ya simu yenye maisha ya kidigitali inayoongoza Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995. Kupitia bidhaa zake mbalimbali za kipekee kwenye sauti, ujumbe mfupi, internet yenye kasi na huduma za kifedha kwenye mitandao ya simu za mikononi , Tigo imekuwa mwanzilishi katika ubunifu wa kidigitali kama vile simu ya kwanza ya smartphone kwa kiswahili, Huduma ya facebook kwenye lugha ya kiswahili, bure, huduma ya TigoPesa, Huduma ya simu ya Tigo pamoja na huduma ya kwanza Afrika Mashariki ya kutuma fedha kwa njia ya simu za mikononi nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili sarafu ya nchi husika.

Kwa taarifa zaidi: woinde.shisael@tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment