Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 18 September 2018

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WATANGAZA KUANZA RASMI KWA SAFARI ZA AIR TANZANIA NCHINI HUMO

Mhe. Balozi Luvanda akitangaza rasmi kuanza kwa safari za Shirika la Ndege la Tanzania nchini India huku picha ya Ndege ya Shirika hilo aina ya Dreamliner ikionekana. Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini (TTB), Bi. Devotha Mdachi ambaye yupo nchini India kushiriki maonesho hayo aliyoshiriki kuandaa anaonekana akichukua kumbukumbu ya tukio hilo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bibi Devotha Mdachi naye akizungumza wakati wa maonesho yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Bodi hiyo.
Ubalozi wa Tanzania nchini India kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania na Shirika la Ndege Tanzania umeandaa Maonesho Maalum ya Utalii na kutambulisha rasmi kuanza kwa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania zitakazofanyika Mjini Mumbai nchini humo kuanzia mwezi Novemba, 2018.

Maonesho hayo ambayo yatafanyika kwenye miji mikubwa mitatau ya India yaani New Delhi, Ahmedabad na Mumbai yanalenga kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nnchini.

Akizungumza wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Hoteli ya Roseate, Aerocity jijini New Delhi, Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda alisema kuwa anaona fahari kubwa kushiriki maonesho hayo muhimu kwa Tanzania na India na alitumia fursa hiyo kutangaza rasmi kuanza wa safari za kwanza za ndege ya shirika la ndege la Tanzania mjini Mumbai.

Balozi Luvanda alisema kuwa safari za ndege hiyo nchini India ni fahari kubwa kwa Tanzania kutokana na ukweli kwamba nchi hizi mbili zina mahusiano ya kihistoria kwani mbali na kuunganishwa na Bahari ya Hindi, Tanzania na India ni marafiki na zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja mbalimbali zikiwemo biashara, utamaduni na mawasiliano ya mtu mmoja mmoja.

Mhe. Balozi Luvanda alisisitiza kuwa, safari za ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania nchini India hususan katika mji wa Mumbai zitaimarisha sekta ya utalii nchini kwa kuongeza idadai ya watalii kutoka nchini humo ambao kwa sasa takribani watalii 40,000 kutoka nchini humo wanatembelea Tanzania kwa mwaka. Pia zitarahisha safari za wanafunzi wa kitanzania wanaosoma kwenye vyuo vikuu mbalimbali vya India ambao idadi yao imeongezeka na kufikia 2500 kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment