Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 19 September 2018

TIGO NA CLOUDS WAZINDUA MSIMU WA TIGO FIESTA 2018 – VIBE KAMA LOTE

Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar Es salaam katika uzinduzi wa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 nchini, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati).
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote kupata vibali kutoka kwa baraza hilo. Tigo Fiesta 2018 inatarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 nchini, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia). 
Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote unaotarajiwa kuwapa fursa wasanii wa nyumbani kutoa burudani za muziki katika mikoa 15 ya nchi, kuanzia Morogoro tarehe 29 Septemba. Pamoja naye ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner Habash (katikati) na Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga (kulia).

No comments:

Post a Comment