Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 8 August 2018

VODACOM YAZINDUA HUDUMA MPYA YA MALIPO KWA MFUMO WA SERIKALI WA KIELEKTRONIKI (GePG) KWA KUPITIA M-PESA APP QR CODE

Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya bidhaa na Masoko wa M-Pesa, Vodacom Tanzania Plc, Polycarp Ndekana (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya na ya kwanza nchini inayomwezesha mwananchi kufanya malipo kwa mfumo wa serikali wa Kielektroniki (GePG) kwa kupitia M-Pesa APP QR Code. Huduma hii inamrahishia mteja kufanya malipo kwa uharaka zaidi ambapo zaidi ya taasisi za serikali 150 zinapokea malipo kwa njia ya huduma hiyo kwa kupiga *150*00# wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mhasibu wa Wakala wa 
Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Audiface Cresence na Afisa Mwandamizi wa Tehama Wizara ya Fedha, Benard Mabagala. 
Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya bidhaa na Masoko wa M-Pesa, Vodacom Tanzania Plc, Polycarp Ndekana (kulia) akiwaonyesha waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, (hawapo pichani) jinsi ya kujiunga na huduma ya malipo kwa njia ya mtandao wakati wa uzinduzi wa huduma mpya na ya kwanza nchini inayomwezesha mwananchi kufanya miamala ya malipo kwa mfumo wa serikali wa Kielektroniki (GePG) kwa kupitia M-Pesa APP QR Code. Huduma hii inamuwezesha mteja kufanya miamala haraka zaidi, kwa sasa taasisi za serikali zaidi ya 150 zinapokea malipo kwa njia ya huduma hiyo kwa kupiga *150*00# wanaoshuhudia kutoka kushoto Mhasibu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Audiface Cresence na Afisa Mwandamizi wa Tehama Wizara ya Fedha, Benard Mabagala.
Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya bidhaa na Masoko wa M-Pesa, Vodacom Tanzania Plc, Polycarp Ndekana (katikati), Mhasibu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Audiface Cresence (kushoto) na Afisa Mwandamizi wa Tehama Wizara ya Fedha, Benard Mabagala wakiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) vipeperushi vinavyoonyesha jinsi ya kufanya malipo kwa taasisi za serikali kupitia Huduma ya M-Pesa APP QR Code. Huduma hii mpya na ya kwanza nchini inamwezesha mwananchi kufanya miamala ya malipo kwa mfumo wa serikali wa Kielektroniki (GePG) kwa haraka, zaidi ya taasisi za serikali 150 zinapokea malipo kwa njia ya huduma hiyo kwa kupiga *150*00#
Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya bidhaa na Masoko wa M-Pesa, Vodacom Tanzania Plc, Polycarp Ndekana (kushoto) akimsikiliza Mhasibu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Audiface Cresence (kulia) akiongea na waandishi wa habari, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya na ya kwanza nchini inayomwezesha mwananchi kufanya miamala ya malipo kwa mfumo wa serikali wa Kielektroniki (GePG) kwa kupitia huduma ya M-Pesa APP QR Code. Huduma hii ya haraka zaidi inaokoa muda wa mteja, zaidi ya taasisi za serikali 150 zinapokea malipo kwa njia ya huduma hiyo kwa kupiga *150*00#

No comments:

Post a Comment