Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert

Ultimate Finance Advert

Advertise Here

Advertise Here

Friday, 11 May 2018

BENKI YA EXIM YA INDIA YAIPATIA SERIKALI YA TANZANIA MKOPO WA MASHARTI NAFUU KUSAIDIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KATIKA MIJI 23 YA TANZANIA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi Amina Kh. Shaaban kwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya India, Bw. David Resquinha wakisaini kwa niaba ya Serikali zao Mkataba wa Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 23 ya Tanzania.
Bi. Shaaban na Bw. Resquinha wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kusaini. 
Picha ya pamoja.
Serikali ya India kupitia Benki ya Exim imeipatia Serikali ya Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 500, sawa na shilingi Trilioni 1.14 za Tanzania, kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 23 ya Tanzania.

Hafla ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika jana tarehe 10 Mei, 2018 mjini New Delhi, India ambapo Bi. Amina Kh. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango na Bw. David Resquinha, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim walisaini kwa niaba ya Serikali zao..

Miji itakayonufaika na Fedha za mkopo huu ni Muheza, Makambako, Kayanga, Njombe, Manyoni, Songea, Sikonge, Chunya, Kasulu, Kilwa Masoko, Rujewa, Mugumu, Geita, Makonde, Wangingómbe, Handeni , Singida mjini, Kiomboi, Mpanda, Chemba, Mafinga, Urambo-Kaliua pamoja na miji ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba, Naibu Katibu Mkuu, Bi. Amina Kh. Shaaban, amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa sababu itawezeshaupatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika miji husika hivyo kusaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko yanayotokana na maji yasiyo salama.

Aidha, miradi itasaidia kufikiwa kwa malengo na mipango ya Taifa na Kimataifa ya Maendeleo ikiwemo: Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano awamu ya pili (FYDPII) , Mkakati wa Kukuza na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA III) na Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDG’s).

Vilevile, amesema uamuzi wa Serikali wa kuboresha huduma za maji umelenga kuwapunguzia Wananchi husususan Wanawake adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji, na hivyo kupata muda wa kutosha kufanya shughuli mbali mbali za maendeleo.

No comments:

Post a Comment