Foreign Exchange Rates

CRDB Bank Advert

Ultimate Finance Advert

Advertise Here

Advertise Here

Friday, 9 March 2018

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN MAGUFULI AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHATO MKOANI GEITA - MACHI 9, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita. Machi 9, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi mbalimbali wa Chato waliohudhuria katika ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita. Machi 9, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kuwasili katika sherehe za ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo Chato Mkoani Geita. Machi 9, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay mara baada ya Benki hiyo kuchangia mfuko wa Elimu wa mkoa wa Geita kwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 50 kabla ya ufunguzi wa Tawi hilo la Benki. Machi 9, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Ally Laay pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji wakati wakipiga picha ya pamoja. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma wakati msanii wa Msechu Bendi Peter Msechu alipokuwa akiimba mara baada ya kufungua tawi hilo la Benki. Machi 9,2018.

No comments:

Post a Comment