Mwenyekiti wa bodi ya Finca, Mike Gama-Lobo akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ya 20 ya Taasisi hiyo jijini Dar Es Salaam hivi karibuni. |
FINCA imesisitizia nia yake ya kuendelea kuwa taasisi inayoongoza katika ushirikishaji wa kifedha nchini.
Raisi na Mkurugenzi Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon aliipongeza FINCA Tanzania kwa safari yake yenye mafanikio waliopata ambayo imewafikisha katika miaka 20 ya maendeleo na mabadiliko, yaliyosaidia taasisi hiyo kuendelea kuwa taasisi ya kutoa mikopo midogo na kufikia kuwa Benki ya kutoa mikopo midogo ilivyo sasa.
Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA ambaye pia ni Makamu wa Raisi na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike Gama-Lobo aliwashukuru wajumbe wenzake wa Bodi na viongozi wa juu wa Benki kwa kuonyesha juhudi za kuigwa ambazo zimepelekea katika kukua kwa FINCA, kufikia maendeleo makubwa katika mazingira ya biashara yenye changamoto nyingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya FINCA Microfinance, Tanzania Issa Ngwegwe amesema: "Mafanikio haya ya miaka 20 ni ushuhuda wa hamasa ya FINCA katika kutoa huduma za kifedha zilizokuwa salama na kuwawezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania
Akielezea kuhusu hali ya ukopeshaji ya FINCA, Ngwegwe alisema: "Tangu FINCA ilipoanzishwa mwaka 1998, tumeweza kutoa zaidi ya TZS 900 Billioni katika mikopo kwa wajeja zaidi ya milioni 1.1 wakiwemo wajasiriamali wadogo, kukuza biashara zao, kutengeneza ajira na kuboresha kiwango cha maisha. Katika miaka ijayo, tutaendelea kutekeleza wajibu wetu katika kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo (SMEs) ambao ndio msingi wa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu.
Aliongeza kusema zaidi kwamba FINCA ilikuwa imejidhatiti katika mpango wake wa kuondoa umaskini kupitia suluhisho la kudumu ambalo linasaidia watu kujenga rasilimali zao, kutengeneza ajira na kuboresha kiwango chao cha maisha.
Kuhusu FINCA Microfinance Bank Tanzania
Benki ya FINCA Microfinance Tanzania ni sehemu ya mtandao wa FINCA Impact Finance, Kundi la taasisi zinazotoa mikopo midogo na taasisi za kifedha 21 ambazo zinatoa huduma za kifedha kwa jamii na kusaidia wajasiriamali wenye kipato kidogo na wamiliki wa biashara ndogo kuwekeza kwaajili ya baadae.
Kuhusu FINCA Impact Finance
Mtandao wa FINCA Impact Finance wenye taasisi 21 za kutoa mikopo midogo na mabenki unatoa huduma za kifedha za uwajibikaji ambazo zinawawezesha wajasiriamali wenye kipato kidogo na wamiliki wa biashara ndogo kuwekeza kwaajili ya baadae. Wamiliki wakuu wa mtandao huo ni FINCA International, watoaji wa mikopo midogo midogo na kampuni yakijamii yasiyo ya kibiashara yaliyojikita katika kujenga ushirikishwaji wa kiuchumi kwa watu maskini.
Kwa maelezo zaidi, Tembelea www.FINCAImpact.com
No comments:
Post a Comment