Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 25 January 2018

MWALIMU COMMERCIAL BANK PLC YAZINDUA BIDHAA KWA AJILI YA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA

Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kibenki kwa njia ya Mitandao wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), John Mhina (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko, Valence Luteganya na Meneja Masoko wa benki hiyo, Rahma Ngassa. 
Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Valence Luteganya (wa tatu kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya ‘MCB Salary Advance’ ambayo wateja wanaopitishia mishahara yao katika benki hiyo wataweza kupata mikopo ya hadi nusu ya mishahara yao kuwawezesha kutatua mahitaji yao ya dharura. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Mikopo, Isaya Hagamu, Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa njia ya Mitandao, John Mhina na Meneja Masoko, Rahma Ngassa.
24 JANUARI 2018, Dar es Salaam – Mwalimu Commercial Bank PLC (MCB) imezindua bidhaa iitwayo MCB Salary Advance, ikiwa ni moja ya mkakati wake katika kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla.

Akizungumzia Kuhusu bidhaa hii mpya ya mkopo wa ‘MCB Salary Advance’, Mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara na masoko, Bwana Valence Luteganya alisema, mteja ataweza kuchukua mkopo huu pale anapouhitaji, Nia ni kuwezesha mteja wetu kuyakabili mahitaji ya dharura yanayojitokeza wakati wowote.

Alisema, bidhaa ya salary advance inayowalenga wateja wafanyakazi wanaopitishia mishahara yao katika Benki ya Mwalimu, “Mkopo huu unariba nafuu na unapatikana kwa urahisi na haraka, Lengo ni kutoa mkopo wa bei nafuu utakao wasaidia wateja wetu  kupunguza ukali wa Maisha”.

Aliongeza “Kupitia huduma ya Salary advance mfanyakazi anayepitisha mshahara MCB, ataweza kupata hadi asilimia 50 ya mshahara wake kwa riba nafuu. Kupata huduma hii mteja anatakiwa kutembelea tawi la benki au kutuma meseji kupitia whatsapp kwa kuandika neno ‘mshahara wangu’ kwenda namba 0629331755.

Akiendelea Ndg Luteganya alisema “Hivyo benki hii ya biashara ya Mwalimu imekuja na mikakati ya kutoa bidhaa nzuri zinazokidhi matakwa ya watanzania ili kuisaidia jamii kupunguza na/ama kuondokana na shida ambazo zinaweza kutatuliwa kwa urahisi.

Naye Mkuu wa kitengo cha huduma kwa njia ya mitandao Ndg. John Mhina aliongeza kwa kusema “Huu ni mwendelezo wa mchakato maalum kuhakikisha tunatimiza mahitaji ya wateja wetu  mwaka 2018, na ni ishara kuwa Benki ya Mwalimu imejipanga vyema katika kutoa bidhaa na huduma zinazolenga maslahi ya watanzania hivyo kuufanya mwaka huu kuwa wa neema kwa wateja wetu. Tunakaribisha Watanzania wote kuja kufungua akaunti na kuweza kufaidi huduma na bidhaa zetu.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa:
Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB).
Mlimani Tower - Mezzanine Floor, Sam Nujoma Road
P.O. Box 61002, Dar es Salaam
Telephone: 022-2772954/7 and +255 629 331 151

Email; info@mcb.co.tz

No comments:

Post a Comment