Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 16 September 2017

G-NAKO AWASHIRIKISHA WASHINDI WA MWAGIKA CHALLENGE KWENYE VIDEO YAKE MPYA


Shindano la “Mwagika Challenge” lililoendeshwa na kampuni ya bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager hivi karibuni limefikia tamati ambapo Iddi Kidungwa, Michael Mwalembe na Nasma Msangi wakiibuka washindi. 

Washindi hao wanatarajiwa kuonekana kwenya video mpya ya msanii mkubwa wa bongo Fleva, G-Nako Warawara
‘Mwagika Challenge’ iliyokuwa na lengo la kuwapa fursa vijana kuonesha vipaji vyao pia liliungwa mkono na mastaa kama Shettah na Shilole waliokuwa mstari wa mbele kuhimiza mashabiki kushiriki shindano hilo pia ni miongoni mwa wasanii watakaonekana kwenye video hiyo.


Video hiyo inayotarajiwa kutoka 17.09.2017 itakuwa ya aina yake kutokana na vionjo mbalimbali vilivyotumika. Sitaki kukuchosha na stori nyingi, tizama teaser hapa chini na endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Kilimanjaro kuona safari ya Mwagika challenge hadi kutengeneza video hii.

No comments:

Post a Comment