Foreign Exchange Rates

DStv Advert_010224

DStv Advert_010224

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 18 July 2017

TIGO YAJIONGEZA ZAIDI UBORESHAJI WA MTANDAO

Ofisa Mkuu wa Ufundi na Mawasiliano wa Tigo,Jerome Albou,akizungumza na wahabari mbalimbali jijini Dar es Salaam juzi,Juu ya Uwekezaji katika ku vya habari kwenye warsha ya uwekezaji katika kuboresha upatikanaji wa mtandao wa Tigo kote nchini.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, ambayo ni kinara wa ubunifu wa mitindo ya maisha ya kidijitali nchini, imetangaza mageuzi katika uwekezaji  ili kuboresha upatikanaji wa mtandao ili kuweza kuwapatia huduma bora zaidi wateja wake wa matumizi ya sauti na data.
Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari nchini, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ufundi na mawasiliano wa Tigo, Jerome Albou,amesema  kampuni  hiyo imewekeza kiasi cha dola za kimarekani millioni 75 kwenye mradi mkubwa wa kuendeleza mtandao huo.
Alisema moja ya malengo yao kimkakati ni kubadilisha uzoefu wa wateja kwa kuwapatia mtandao wenye ufanisi kulingana na viwango vya sekta ya mawasiliano ambapo katika miaka mitatu iliyopita Tigo imeweza kuongeza msingi  wa wateja wake kufikia zaidi ya milioni 10.
“Kadri tunavyoendelea kukua, kupanua  mtandao na kuufanya kuwa wa kisasa zaidi, ni jambo la lazima kutoa huduma bora zaidi,” alisema Albou huku akiongeza kwamba kuanzia mwaka jana kampuni ya Tigo imefanya upanuzi mkubwa wa miundo mbinu ili kuweza kufikia maeneo mengi nchini.

“Mahitaji ya matumizi ya data yamekuwa yakiongezeka kila siku, hivyo Tigo imeweza kuhakikisha matumizi ya 3G na 4G yanaweza kuwafikia watumiaji vijijini,” aliongeza Albou.

No comments:

Post a Comment