Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Wednesday 14 June 2017

WAZIRI MKUU MH. KASSIM MAJALIWA APONGEZA UKARIMU WA VODACOM TANZANIA FOUNDATION

Mh. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (katikati) akishuhudia Shekh mkuu wa Ruangwa mkoa wa Lindi akipokea boksi lenye tende kwa niaba ya watoto wanaoshi katika mazingira magumu mkoani hapo toka kwa Meneja mauzo wa mkoa huh  Omary Kilumanga na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu baada ya kufuturu futari mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania Foundation mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiongea na wakazi wa Ruangwa mkoa wa Lindi mara baada ya kufuturu futari mwishoni mwa wiki iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania Foundation mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameipongeza Vodacom Tanzania Foundation kwa kuendelea kuwafuturisha watoto na wazee waishio katika mazingira magumu nchini.

Mh. Waziri Mkuu ameyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Ruangwa Lindi katika futari iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania Foundation mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kujitolea katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Huu ni mwendelezo wa kampeni ya “Ukarimu wa Vodacom” ambayo ina lengo la ukarimu, ushirika na utoaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na katika maisha ya kila siku.

Huduma hii yenye lengo la kuendeleza mshikamano inakwenda sambamba na kuwawezesha Waislamu na Watanzania kwa ujumla wao kujiunga na kifurushi kinachowapatia muda wa maongezi, SMS na kuwawezesha kupiga simu BURE wakati wakisubiri muda wa kula daku, kugawa tende pamoja na maji. Pia huduma hiyo inawakumbusha muda wa kuswali na kuwapatia Mawaidha na Hadith. Ili kujiunga na huduma hii mteja anapiga *149*01# kisha anachagua aina ya bando kulingana na uwezo wake wa kifedha, kuna bando linalodumu kwa saa 24 na lingine linadumu kwa siku 7.

No comments:

Post a Comment