Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe: Charles Mwijage akizungumza wakati wa mkutano huo.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
WIZARA ya Viwanda na biashara kupitia kituo cha uwekezaji (TIC) wameingia makubaliano na wataalamu nguli wa utafiti kuanisha fursa zote zilizopo nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji ,Charles Mwijage amesema kuwa wataalamu hao wataweza kutusaidia kuto ahabari za kutosha juu ya fursa zilizopo hapa nchini.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic akizungumza katika hafla hiyo.
“Sijaridhika na namna tunavyojitangaza hivyo tunapashwa kuandika habari nyingi juu vitu tulivyonavyo hasa hzi fursa kupita majarida makubwa duniani na vyombo mbalimbali vya habari” Amesema Mwijage.
Ameitaka tasisi hiyo kutengeneza kitu ambacho watanzania awawezi kutengeneza na kufikisha mahali ambapo wataalamu wetu awawezi kufikisha kwa uraisi lakini wao watafika na kusikilizwa.
Waziri Mwijage ametaja kuwa mara baada ya Asia kukua katika uwekezaji sehemu iliyobaki ni Afrika na nchi yenyewe ni Tanzania ambapo kuna kila namna na mazingira ya uwekezaji kwa tasisi za nje.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari (kulia) akishikama mkono na Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic mara baada ya kuaisiana makubaliano ya kiutafiti katika kuanisha fursa mbalimbali zilizopo nchini, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mitutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake mkurugenzi wa TIC, Clifford Tandari amemuakikishia waziri kuwa watalaam hao wana uwezo wa hali ya juu na watawaeza kutengeza kitu ambacho watalaamu wetu awawezi pia kupitia mtandao wa unaofahamika ulimwenguni wataweza kuinganisha mtandao wa TIC hili kila mtu apate kujionea vitu vilivyopo hapa nchini.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (katikati) akizungumza jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford Tandari. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Oxford Business Group, Ivana Carapic.
Baadhi ya Watendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini wakifatilia mkutano huo.
No comments:
Post a Comment