Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday 20 October 2016

SIMBA CEMENT YAZIPIGA TAFU SHULE TATU TANGA KUPUNGUZA KERO YA MADAWATI

Mkuu wa Idara ya Rasilimali watu kiwanda cha Tanga Cement (Simba Cement), Dianna Malambugi (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwailapwa, madawati 100 kwa shule tatu za msingi, Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martin Shamba za halmashauri ya jiji la Tanga kupunguza uhaba wa madawati na wanafunzi kusomea chini. 


Kufuatia Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu. 
Shule hizo ambazo zimefaidika na mpango huo ni Magaoni, Kiruku, Mkombozi na Martini Shamba zote za halmashauri ya jiji la Tanga.
Akizungumza wakati wa makabidhiano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga , Thobias Mwailapwa, Mkuu wa Idara Rasilimali watu kiwabda cha Saruji , Diana Malambusi amesema msaada huo umekuja baada ya kuona kero ya wanafunzi kusomea chini kutoisha. 

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano, Mkuu wa Wilaya, Thobias Mwailapwa, amekishukuru kiwanda hicho (Simba Cement) na kuyataka mashirika na taasisi pamoja na makampuni kuiga mfano huo ili kumaliza kero ya wanafunzi kusomea chini. 

Kwa upande wake Afisa elimu shule ya msingi jiji , Khalifa Shemahonge, amesema madawati hayo yatatumika kama inavyokusudiwa na kuahidi kuyatunza ili kuongeza uelewa wa wanafunzi darasani. 

No comments:

Post a Comment