Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Thursday, 6 October 2016

NIGERIA KUUZA NDEGE ZA RAIS KUBANA MATUMIZI

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

ABUJA-NIGERIA, RAIS wa Nigeria, Muhammadu Buhari, amefanya uamuzi wa kuuza ndege mbili za rais kati ya 10 ikiwa ni hatua ya kupunguza matumizi ya serikali.

Buhari, mwenye umri wa miaka 73 aliyeingia Ikulu ya Nigeria mwaka jana, amekuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo viovu nchini mwake, na hasa vita dhidi ya rushwa.
Mtandao wa habari wa Reuters umemkariri Msemaji wa Rais Buhari, Garba Shehu, akiweka bayana kwamba rais wa taifa hilo tajiri kwa mafuta ametumia mamlaka yake kufanya uamuzi huo wa kuuza ndege hizo.

"Huu ni uamuzi wa Rais Muhammadu Buhari ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kupunguza matumizi yasiyo ya lazima," anasema Shehu.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za kiuchumi, Nigeria imekuwa katika mdororo uchumi mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 20 hivi, sababu kuu ya hali hiyo ikiwa ni kuporomoka kwa bei ya mafuta duniani.

Mauzo ya mafuta ghafi nchini Nigeria, ambayo huuzwa nje ya nchi hiyo huchangia asilimia 70 ya mapato ya serikali na kwa hiyo, kwa vyovyote vile, ni lazima mtikisiko katika biashara ya mafuta utikise pia uchumi wa taifa hilo.
Mwisho








No comments:

Post a Comment