Foreign Exchange Rates

Ascon Africa advert_6th Dec. 2018

Stanbic Bank - Uhuru Banking - 5th Nov. 2018

CMTL Advert - 5th Nov. 2018

Friday, 28 October 2016

BENKI YA EXIM YABORESHA HUDUMA KWA WATEJA WAKE, WAZINDUA TAWI LA TEMEKE JIJINI DAR.

Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda akishirikiana na wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Temeke kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi la Temeke jijini Dar es Salaam.

BENKI ya Exim imefanya maboresho ya huduma zinazotolewa kwa wateja wake wa maeneo ya Temeke, jijini Dar es Salaam kwa kufungua tawi jipya ambalo lina maboresho mengi tofauti na jengo ambalo walikuwa wakilitumia awali.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda amesema kwasasa wamedhamiria kuboresha huduma zao katika maeneo mbalimbali na kuahidi wateja kuendelea kuwapatia huduma bora. 

“Benki yetu inaendelea kufanya vizuri na tumejipanga kuendelea kuboresha huduma zetu, mwanzoni tulikuwa sehemu nyingine na wateja wetu walikuwa wakituuliza lini tutahamia sehemu iliyo na nafasi nzuri ya kutoa huduma na sasa tumeipata,” alisema Mponda. 
Wageni waalikwa wakikata keki. Wa kwanza kushoto (mwenye suti nyeusi) ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, Seleman Mponda, Mteja wa Benki ya Exim, Abdelsamad Hussein, Afisa Mauzo wa Benki ya Exim Temeke, Rashid Bundara, Mteja wa Benki ya Exim, Saamu Omary, Mteja wa Benki ya Exim, Shukran Ezekiel.

No comments:

Post a Comment