Mrembo wa taji la Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wageni walikwa pamoja na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa duka lake la samani za ndani "Amorette" lililopo katika jengo la Village Walk gorofa ya kwanza karibu na Sea Cliff Hotel, Masaki jijini Dar es Salaam. |
Akizungumzia duka hilo, Bi. Mengi alisema kuwa ilikuwa ni ndoto yake ya muda mrefu ya kutaka siku moja kuwa na duka kama hilo ambalo litakuwa na samani ambazo ni ngumu kuzipata sehemu nyingine kutokana na kutengenezwa tofauti na samani nyingi ambazo zinapatikana madukani.
"Siamini kama ndoto yangu imetia, kwa kipindi cha miaka iliyopita kuna vitu nilikuwa nikitamani kuwa navyo nyumbani lakini sikuweza kuvipata nilipokuwa nikitafuta na hapo ndipo ndoto za kuwa na duka zilipoanzia,
"Nilikuwa nataka kitu cha tofauti ambacho ni ngumu kukikuta sehemu nyingine kutokana na kuwa na ubunifu wa kipekee ambao utawavutia wateja wa ndani ya nchi na nje ya nchi na ninaamini watafurahia," alisema Bi. Mengi.
Aidha Bi. Mengi alisema kuwa bidhaa ambazo zitakuwa zikipatikana katika duka la Molocaho - Amorette zimetengenezwa na malighafi kutoka Tanzania kama mbao za Mninga na hivyo kuwataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kutumia bidaa ambayo imetengenezwa na malighafi za Tanzania.
Mmoja wa wageni waliohudhuria halfa ya uzinduzi, Faraja Nyalandu alisema kuwa kwa kijana kama Jacqueline Mengi kuwa na duka kama hilo ni hatua kubwa ambayo vijana wengi wanatamani kuifikia, kumpongeza kwa juhudi alizozifanya lakini pia kutoa ushauri kwa wengine ambao wanataka kufanikiwa.
"Kwanza nimpongeze Jacqueline amefanya uthubutu na amefanikiwa kuwa na kitu kama hiki, juhudi yake inaonyesha kuwa kila mtu tu anaweza kufanikiwa kama akiongeza juhudi katika jambo analotaka kulifanya," alisema Bi. Nyalandu.
Duka hilo la kisasa na la aina yake linapatikana Masaki karibu na hoteli ya Sea Cliff kwenye jengo la "Village Walk" gorofa ya kwanza.
Muonekano wa nje utaokutambulisha hili ndio duka la "Amorette".
|
Bi. Jacqueline Mengi akikata utepe kuzindua duka lake hilo. |
Ha ha ha ha, sasa mko huru kuingia wageni waalikwa kujionea yaliyomo,.....Bi. Jacqueline Mengi akifurahi jambo mara baada ya kukata utepe.
|
Bi. Jacqueline Mengi akiongozana na baadhi ya wageni waalikwa kuingia ndani ya duka la "Amorette". |
Balozi Juma Mwapachu na baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia moja ya meza ya chakula (dining table) iliyotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga baada ya kuzinduliwa duka hilo lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar. |
Wageni waalikwa wakiendelea kukagua samani mbalimbali katika duka hilo. |
Bi. Jacqueline Mengi akiwaonyesha mambo mazuri yaliyomo katika duka la Amorette baadhi marafiki waliohudhuria uzinduzi huo.
|
Bi. Jacqueline Mengi akizungumza jambo na Balozi Juma Mwapachu wakati akiwatembeza wageni waalikwa katika maeneo mbalimbali ndani ya duka lake la Amorette. |
Wageni waalika wakiangalia moja ya kitanda cha aina yake kinachouzwa katika duka la Amorette lililopo katika jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es Salaam. |
Sehemu maalum ya kitanda hicho ya kuhifadhia mashuka, Blanket pamoja na mito. |
Bi. Jacqueline Mengi akipozi katika moja ya samani ndani ya duka lake la Amorette. |
Bi. Jacqueline Mengi katika pozi matata ndani ya duka lake la Amorette. |
Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua duka lake la samani za ndani la Amorette. |
Wanahabari na wageni waalikwa wakiwa ndani ya duka la Amorette kujionea bidhaa mbalimbali. |
Wageni waalikwa wakiendelea kutazama kitanda hicho cha aina yake. |
Sophia Byanaku akijinafasi katika moja ya samani zilizomo kwenye duka la Amorette.
Mmoja wa wageni waalikwa akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kwa mbao aina ya Mninga ndani ya duka la Amorette.
|
Balozi Juma Mwapachu (kushoto) akibadilishana mawazo na mwalikwa mwenzake kwenye uzinduzi wa duka la Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akipozi kwenye samani moja wapo inayopatikana katika duka lake la Amorette.
Warembo wakiwa wamepozi kwenye samani zinazopatikana katika duka la Amorette lililopo ndani ya jengo la Village Walk, Masaki jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo ndani ya duka la Molocaho-Amorette.
Bi. Jacqueline Mengi akiwa kwenye picha ya pamoja na rafiki zake.
Bi. Jacqueline Mengi akibadilishana mawazo na baadhi ya marafiki zake.
Mkurugenzi wa Dorice Mollel Foundation, Dorice Mollel (kulia) katika picha ya pamoja na Mdau Monica Joseph.
Bi. Jacqueline Mengi katika picha ya pamoja na Dorice Mollel.
No comments:
Post a Comment