Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Friday, 8 July 2016

WASHINDI WANNE WANYAKUA ZAWADI KATIKA KAMPENI YA FAIDIKA NA AMANA BANK

Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi ya Television mshindi wa kwanza wa kampeni ya Faidika na Amana Bank Bi PIKIRA NLONGANE wakati wa Hitimisho la kampeni hiyo iliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo watanzania wa kuwekeza zaidi. Hitimisho la Kampeni hiyo limefanyika wakati wa siku ya maonyesho ya kimataifa ya biashara saba saba Jijini Dar es salaam ambayo Bank ya amana ni moja kati ya wafanyabiashara waliokuwa na Banda katika Maonyesho hayo .
Zawadi ya JOKOFU kwenda kwa mshindi wa pili ambaye ni SHAKIRA IBRAHIMU imekabidhiwa na kupokelewa na mwakilishi wake ambaye ni AHMED SANDE (Pichani) akikabidhiwa zawadi hiyo na Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD wakati wa utoaji wa zawadi hizo.
Mshindi wa nne amepata zawadi ya Table Feni ya kisasa yenye AC pia. Pichani ni Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akimkabidhi zawadi Bwana HEMED SULEIMAN ambaye ameibuka mshindi wa nne katika kampeni ya Faidika na Amana Bank iliyochezeshwa ndani ya banda la Bank hiyo katika maonyesho ya kimataifa ya Biashara ya saba saba Jijini Dar es salaam ambapo washindi wanne wamejinyakulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi za kitanzania Million Tano.
Mkurugenzi wa Bank ya Amana DR MUHSIN MASOUD akizungumza na wanahabari wakati wa Utoaji wa zawadi hizo kwa washindi wanne wa Kampeni ya Faidika na Amana Bank ambapo amewataka watanzania kuwa na utamaduni wa kuwekeza kwani ni utamaduni mzuri na unaofaa kuendelezwa.
Meneja masoko wa Bank ya Amana Ndugu DASSU MUSSA akifafanua jambo kwa wanahabari ambao walifika kushughudia Utoaji wa zawadi hizo katika Banda lao lililopo katika maonyesho ya saba saba ambayo ndiyo yanaelekea ukingoni.
Zawadi ambazo zimetolea kwa washindina Bank ya Amana ambazo jumla zimegharimu kiasi cha shilingi million Tano.
Picha ya Pamoja maafisa wa Bank ya Amana wakiwa na washindi wa zawadi mbalimbali za kampeni ya Faidika na Amana Bank mara baada ya utoaji wa zawadi hizo katika maonyesho ya Saba saba.

No comments:

Post a Comment