Maonesho ya ya bidhaa za viwandani yatakuwa na manufaa zaidi kwa Tanzania iwapo makampuni Makubwa ya kutoka nje ya nchi yatazalisha bidhaa hizo hapa hapa nchini.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini - TPSF Dr. Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita wakati akifungua maonesho ya siku tatu ya Mafuta na Gesi yaliyoratibiwa na Kampuni ya EXPOGROUP, kwa kushirikiana na TPSF.
Amesema Maonesho ya aina hiyo ni mazuri kwa kuwa yanatambulisha bidhaa na teknolojia mpya sokoni. Hata hivyo amesema Watanzania hawapaswi kuwa watazamaji tu, bali watumie mwanya huo kuyashawishi makampuni hayo kutengeneza bidhaa zao hapa hapa nchini.
Baada ya uzinduzi wa maonesho hayo, na machapisho yake, Dr Mengi, aliyefuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye, walitembelea baadhi ya mabanda ya maonyesho kujionea bidhaa mbalimbali.
Mapema Meneja wa Maonesho hayo yanayoshirikisha makampuni 80 kutoka nchi 24 duniani Bw. Neville Trindade na Afisa Uendeshaji wa EXPOGROUP BW. Pius Gechamet wamesema lengo la maonyesho hayo ni kuvutia uwekezaji na wamewataka Watanzania kuchangamkia maonyesho hayo yatakayodumu kwa siku tatu.
Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Reginald Mengi akizungumza katika maonyesho hayo. |
Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Reginald Mengi akizindua kijarida katika maonyesho hayo. |
Mgeni Rasmi katika maonyesho ya Bidhaa za Mafuta na Gesi yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, Reginald Mengi akizungumza katika maonyesho hayo. |
No comments:
Post a Comment