Kitomari Banking & Finance Blog is a premier site for banking, finance, business, economic, investment and stock market news as well as selected informative articles from Tanzania, East Africa and the rest of the World. We operate 24 hours a day, 365 days a year with complete context, perspective and precision.
Wednesday, 9 September 2015
HUDUMA YA TIGO PESA KUSITISHWA KWAAJILI YA UBORESHAJI
Dar es Salaam Septemba, 7, 2015, Kampuni ya simu ya Tigo Tanzania itasitisha huduma zake maarufu za kutuma na kupokea fedha ya Tigo Pesa wikendi hii kwa muda wa saa 17 ili kufanya maboresho ya huduma hiyo.
Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kampuni ya simu leo jijini Dar es Salaam inasema kuwa kusitishwa kwa huduma ya Tigo Pesa kuanzia Jumamosi usiku hadi Jumapili mchana utakuwa mwendelezo wa zoezi la uboreshaji wa huduma za kifedha za simu kwa takribani siku saba, “ kuifanya huduma ya Tigo Pesa kuwa ya kasi, imara na rahisi kupatikana.”
Huduma za Tigo Pesa zitakazo athirika kutokana na zoezi la marekebisho ni pamoja na ubadilishaji wa nenol a siri na usajili wa wateja wapya ambazo hazitakuwepo kuanzia Septemba 8 hadi 15, ubadilishaji namba ya simu kuanzia Septemba 12 hadi 15 na uboreshaji wa simu utakosekana kuanzia Septemba 6 hadi 16
“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi chote tutakapokuwa tukipambana kukuboreshea huduma yako ya Tigo Pesa kuwa ya kasi, imara na upatikanaji rahisi,” ilisema sehemu ya habari hio. Taarifa inayofanana na hii imechapishwa kwenye vyombo vya habari pamoja na kwenye mitandao ya kijamii.
Tigo Pesa ni huduma maarufu ya kifedha kwa njia ya simu za mkononi nchini Tanzania ikiwa na zaidi ya wateja zaidi ya milioni 4 kote nchini.Huduma zinazotolewa na Tigo Pesa ni pamoja na ubadilishanaji wa fedha kati ya wateja wanaotumia mtandao wa Tigo na kati ya wale watumiao mitandao mingine, pia uhamishaji wa pesa kutoka kwenye simu kwenda Benki na kutoka Benki kwenda kwenye simu.
Mwaka uliopita Tigo Pesa ilikuwa huduma ya kwanza ya kifedha kwa njia ya simu duniani kwa kuvuka mipaka na kuwezesha uhamishaji wa fedha iliyobadilishwa kwenda Rwanda na pia kuwa huduma ya kwanza ya kifedha kwa njia ya simu duniani kwa kutoa gawio la faida kwa wateja wake kulingana na kiasi cha fedha walichokihifadhi kwenye mfuko wao wa Tigo Pesa.
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa ubunifu nchini, inafahamika kama kampuni inayolenga kuleta maisha ya kidijitali katika jamii. Inatoa huduma tofauti tofauti za mawaliano kwa njia ya simu, intanet ya kasi na kutuma na kupokea fedha. Aidha Tigo imebuni bidhaa na huduma mbali mbali kama Facebook kwa Kiswahili, Tigo Pesa App kwa watumiaji wa simu za Android na iOS, na ni kampuni ya simu ya kwanza Afrika Mashariki kuanzisha huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu kimataifa, yenye uwezo wa kubadilisha fedha za kigeni.
Kwa kutumia tekinolojia ya 3G Tigo ina wahakikisha wateja upatikanaji wa huduma bora na za uhakika. Kati ya mwaka 2013 na 2014, kampuni ilizindua minara mipya zaidi ya 500 na pia ina mipango wa kuongeza mara mbili kiwango cha uwekezaji ifikapo mwaka 2017 ili kuweza kupanua wigo wa mawasiliano na uwezo wa mtandao hasa hasa katika maeneo ya vijijini. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 8 na inatoa ajira za moja kwa moja na kwa namna mbali mbali kwa Watanzania zaidi ya 100,000 ambao wanajumuisha wafanyakazi wa huduma kwa wateja, wa kutuma na kupokea fedha, watu wa mauzo pamoja na wasambazaji.
Tigo ni kampuni ya simu inayoongoza chini ya kampuni mama ya mawasiliano Millicom, ambayo imejizatiti katika kuhamasisha na kufanikisha maisha ya kidijitali katika nchi 44 zenye biashara zake Afrika na Latin Amerika, pamoja na ofisi za kampuni zilizopo Ulaya na Marekani. Kwa kutambua kwamba ubunifu ndio utakaowafanya kuendelea kuwa juu ya ushindani, Millicom inaendelea kuthamini mchango wa wadau wake, wakitumia dhana ya “demand more” kama namna ya kufanya biashara na kuendeleza nafasi yao kama kampuni inayoongoza katika kufanikisha maisha ya kidijitali katika baadhi ya masoko makubwa yenye ushindani mkali duniani.
“TABASAMU, UKO NA TIGO”
Kwa maelezo zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na:
John Wanyancha – Meneja Mawasiliano
Simu: 0658 123 089
john.wanyancha@tigo.co.tz
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment