Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Tuesday 4 August 2015

TAMASHA LA NHC FAMILY DAY LAFANYIKA KUNDUCHI BEACH HOTEL

Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo akimkabidhi kombe la ushindi wa kuvuta kamba kapteni wa timu ya kuvuta kamba ya NHC Kinondoni baada ya kuibuka mabigwa katika Bonanza la michezo ya Familia lililofanyika Kunduchi Beach Wet and wild.
Kikosi cha wasimamizi wa michezo ya Bonanza hilo la familia la NHC kikiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu wa Shirika la Nyumba la Taifa, James Rhombo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa, Susan Omari.
Daktari akitoa somo katika Bonanza hilo.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu cha mojawapo ya timu zilizochuana katika Bonanza hilo kikiwa katika picha ya pamoja.
Penati.
Wakiwa katika mazoezi ya pamoja kupasha misuli. Shirika la Nyumba la Taifa linayo Gym maalumu kwa wafanyakazi yenye vifaa vya kutosha vya kisasa kwaajili ya wafanyakazi kujiweka sawa kiafya.
Wafanyakazi wakiendelea na michezo ya Volleyball.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano wa NHC, Bi Susan Omari akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo waliokuwa wakisimamia michezo mbalimbali wakati wa tamasha la NHC Family Day lililofanyika kwenye hoteli ya Kunduchi Beach mwishoni mwa wiki likishirikisha wafanyakazi wa shirika hilo jijini Dar es salaam na familia zao na kufahamiana ikiwani pamoja na kubadilishana mawazo.
Wafanyakazi hao wakishindana katika mbio ufukweni.
Mmoja wa wafanyakazi wa NHC akiwa amejishindia Jogoo katika shindano la kufukuza kuku.
Baadhi ya wafanyakazi wakijiandaa kushindana katika mbio za magunia.
Wakichuana vikali katika mbio za magunia.
Lazima kitoweo kikamatwe hapa.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano wa NHC, Bi Susan Omari akishiriki katika kusimamia upangaji wa timu za mpira wa miguu.
Walishiriki pia katika mchezo huu ambao niliwahi kuucheza sana nikiwa mtoto.
Mchuano wa kuvuta kamba.
Baadhi ya wafanyakazi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa michezo hiyo.

No comments:

Post a Comment