Meneja Afya na Usalama wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Alfred Anthony (kushoto), akizungumza katika semina ya utengenezaji wa matofali iliyoandaliwa na kampuni hiyo ambapo zaidi ya watengeneza matofali 200 walifundishwa jinsi ya utengenezaji bora wa tofali, masuala ya afya na usalama kazini na biashara ya bidhaa hiyo. Semina hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kushoto kwake ni Mhandisi Emmanuel Owoya, Meneja Usambazaji, Tumaini Joseph na Mkurugenzi wa Biashara, Simon Delens. |
No comments:
Post a Comment