Foreign Exchange Rates

DStv Advert_020324

DStv Advert_020324

SBT Tanzania Advert_291123

Saturday 4 April 2015

BENKI YA NMB YADHAMINI MKUTANO WA SERIKALI ZA MITAAKWA SH. MILIONI 200

Benki ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa serikali za mitaa (ALAT) utakaoanza tarehe 8 April mpaka Tarehe 11 April, 2015 katika hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. NMB imetoa shilingi milioni 150 kwaajili ya kufanikisha mkutano huo na shilingi milioni 50 kwaajili ya ununuzi wa trekta litakalotolewa kama zawadi kwa meya (Mayors Award) na halmashauri iliyofanya vizuri katika Nyanja mbalimbali kama utawala bora na utengenezaji wa miradi ya kiuchumi.

Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akitangaza udhamini wa NMB katika mkutano mkuu wa ALAT Taifa mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Karijee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi na pembeni ni Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw Abraham Shamumoyo.
Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi akitangaza maadhimisho ya mkutano mkuu wa 30 wa ALAT -2015. Pembeni ni Afisa Mkuu Fedha wa NMB – Waziri Barnabas na Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw. Abraham Shamumoyo.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akikabidhi mfano wa hundi kwaajili yaudhamini wa mkutano mkuu wa ALAT – 2015 kwa mwenyekiti wa ALAT taifa na meya wa Jiji la Dar es Salaam Dr Didas Masaburi . Katikati ni Katibu Mtendaji wa ALAT – Bw Abraham Shamumoyo.


No comments:

Post a Comment