Foreign Exchange Rates

DStv Advert_090724

DStv Advert_090724

SBT Tanzania Advert_291123

Sunday, 15 March 2015

TANGA CEMENT YATOA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO KAHAMA

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufuga (katikati) akipokea sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya sh milioni 17 kutoka kwa Meneja Biashara wa Kampuni ya Saruji Tanga (Tanga Cement Plc), Mattheus Roos vilivyotolewa na kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mvua ya mawe iliyotokea wilayani Kahama hivi karibuni. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wilayani humo juzi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tanga Cement wakibeba boksi lenye lililokuwa na baadhi ya vitu walivyotoa msaada kwa waathirika wa mvua yam awe iliyotokea wilani Kahama hivi karibuni. Hafla hiyo ilifanyika Kahama, Shinyanga juzi. Kushoto ni Meneja Biashara wa Tanga Cement, Mattheus Roos.
Meneja Mawasiliano wa Huduma za Jamii wa Tanga Cement Plc, Bi. Mtanga Noor (kushoto) akizungumza wakati wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 17 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea wilayani Kahama hivi karibu. Hafla hiyo ilifanyika Kahama, Shinyanga juzi. Kushoto kwake ni Meneja Biashara wa Tanga Cement, Mattheus Roos na Meneja Mauzo Taifa wa kampuni hiyo, Leslie Massawe na baadhi ya wafanyakazi wenzao.
Meneja Biashara wa Kampuni ya Saruji Tanga (Tanga Cement Plc), Mattheus Roos (kushoto), akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh milioni 17 kwa ajili ya wahanga wa mafuriko yaliyotokea wilayani Kahama hivi karibu. Hafla hiyo ilifanyika Kahama, Shinyanga juzi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanga Cement wakiwa katika hfla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Tanga Cement wakiwa katika hfla hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Tanga Cement akizungumza hiyo walipokwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali kusaidia waathirika wa mvua yam awe iliyotokea Kahama hivi karibuni. Walikabidhi vyakula kama mchele, mafuta ya kupikia, maji, unga wa mahindi na ngano, nguo na vitabu vyote vikiwana thamani ya zaidi ya sh milioni 17.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya (kushoto), akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kampuni ya Tanga Cement kusaidia waathirika wa mvua yam awe iliyotokea wilayani humo hivi karibuni. Hafla hiyo ilifanyika Kahama, Shinyanga juzi.

No comments:

Post a Comment